Morogoro: Kundi la tembo lavamia makazi na mashamba na kufanya uharibifu tena

Morogoro: Kundi la tembo lavamia makazi na mashamba na kufanya uharibifu tena

philltaya

Member
Joined
Sep 5, 2015
Posts
53
Reaction score
11
Makundi ya Tembo yamevamia katika baadhi ya vijiji vya kata ya Lubungo wilayani Mvomero kijiji cha vianzi kitongoji cha Menge mkoani Morogoro na kuharibu mazao kwa mara nyingine tena.

Mmoja wa waathiriwa na Tembo hao Bwn Jeremiah Tayari na Bwan Mwombeki wamesena hii ni mara ya pili sasa kutokea kwa uharibifu huo tembo wamemaliza chakula chote walichotegemea, taarifa zimefika katika ngazi husika lakini hawaoni jitahada ya kuona kama kuna uwezekano wa kutatua tatizo hilo.

Tembo hao wanadaiwa kuvamia kwenye maeneo hayo mara kwa mara na kufanya uharibifu wa mazao ambao wanadaiwa huenda wakawa wanatoka hifadhini, lakini kwa awamu hii tembo wamekuwa wengi zaidi kuliko kawaida ya awamu zilizopita.
 
Wawauwe tu kama wale ngamia wa Australia
Au watatulaumu kwa maamuzi magumu[emoji3064]


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
tembo wametoa 'reaction' , naimani kuna 'action' ilifanyika dhidi ya hao tembo
 
Sema watu wa Moro siyo watundu,Hao tembo wanapigiwa Firimbi wanatulia wenyewe Alaf unawarudisha kirivasi rivasi huko walikotoka.
 
Back
Top Bottom