Morogoro: Lori lagonga nyumba, laua watu watatu

Morogoro: Lori lagonga nyumba, laua watu watatu

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Watu watatu ambao ni Wanaume wawili na Mwanamke mmoja wamefariki na mmoja kujeruhiwa katika ajali ya gari baada ya Lori kuacha njia na kuingia katika nyumba iliyo karibu na barabara Mikumi Barabara ya Morogoro-Iringa.

Majeruhi Rajabu Kapomba amesema ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo machi 25 mwaka huu baada ya Lori hilo lenye tela namba za Usajili T.947BQB lililokuaa litokea Songea kuelekea Dar es salaam kufeli brenki na kugonga nyumba.

Daktari wa zamu hospitali ya St. Kizito Mikumi Simon Veda kwenye mahojiano na @ayotv_ amethibitisha kupokea miili ya Watu hao watatu akiwemo Dereva, abiria mmoja na Mtembea kwa miguu huku majeruhi akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

277149970_505356394447186_919558685806121706_n.jpg


Chanzo: Millard Ayo
 
Ndio mana sipendi kabisa..kujenga nyumba karibu na highways.

#MaendeleoHayanaChama
 
Watu wa Mungu ombeeni sana nchi yetu.Hizo ajali mbalimbali zinazotokea TZ kwa sehemu kubwa zinasababishwa na mapepo.
 
Back
Top Bottom