MOROGORO. Makao Makuu ya Kwanza ya Uhamishoni ya ANC.

MOROGORO. Makao Makuu ya Kwanza ya Uhamishoni ya ANC.

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
..katika kupekua-pekua kwenye mtandao nimekutana na kipande cha historia.

..Morogoro ndiyo makao makuu ya kwanza ya ANC uhamishoni.

..hii ni kabla ya ANC kuhamia Lusaka.

..makao makuu ya Umkhonto We Sizwe[ majeshi ya ANC] yalikuwa Kongwa.

..mwaka 1969 kulitokea mfarakano kati ya Tanzania na ANC na kupelekea "kufukuzwa" kutoka Tanzania.

..mfarakano huo ulitokana na tuhuma za ANC kushirikiana na Oscar Kambona kutaka kumpindua Mwalimu Nyerere.

..kutokana na mfarakano huo Tanzania iliwatimua wapiganaji wa ANC, na hivyo kupelekea makao makuu ya ANC kuhamia Lusaka, Zambia.

..kidogo kidogo mahusiano yetu yalirejeshwa ambapo Tanzania ilipokea tena vijana wa ANC kati ya 1972 to 73.

NB:

..kutokana na kupokea kwetu wakimbizi toka kwa ndugu zetu wa Kusini mwa Afrika, Tanzania ilipata kushambuliwa na Makaburu wa Afrika Kusini. Kuna matukio matatu ambayo nimepata kuyasikia. Tukio la kwanza ni shambulizi la manowari za Afrika Kusini zilizoingia Dsm. Tukio la pili ni kuwekwa sumu ktk Mto Ngerengere ambao ulikuwa chanzo cha maji kwenda kwenye kambi la ANC. Tukio la tatu ni jaribio la utekaji nyara wa ndege lililofanywa na kaburu aliyekuwa akifundisha askari wa Umkhonto We Sizwe. Nadhani ilikuwa ni ndege ya Zambia lakini ndege hiyo ililazimika kutua Dsm baada ya vijana wa ANC kumzidi nguvu kaburu huyo na kumkabidhi kwa wanausalama wa Tz.

cc Jasusi, Echolima, EMT, NasDaz, Kichuguu, Shwari, Echolima, Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Ben Saanane, Mohamedi Mtoi, Mag3, MwanaDiwani
 
JokaKuu,
Mbona sielewi? Unasema Morogoro ndio Makao Makuu ya kwanza ya ANC uhamishoni halafu tena unaitaja Kongwa!! Kongwa si upo Dodoma? Morogoro nafahamu ni kweli ANC walikuwa Mazimbu ambayo kwa sasa inatumika kama moja ya kampasi za Sokoine University of Agriculture. Kimsingi, Mazimbu(moja ya Kata za Morogoro Mjini) kilikuwa ni chuo ambacho kilikuwa kinaitwa Solomon Mahlangu Freedom College ambacho kilianzishwa baada ya Soweto Uprising in June 16, 1976' siku ambayo hadi leo inasherehekewa (since 1991) Afrika kama Siku ya Mtoto wa Afrika. Baada ya ile Uprising, wengi walitoroka, na waliokuja Tanzania, hususani vijana (Uprising yenyewe ikihusisha zaidi vijana wanafunzi) ndio waliwekewa chuo pale Mazimbu enzi za Anna Abdallah kama Mkuu wa Mkoa wa Morogoro! Pamoja na Mazimbu, walitengewa eneo lingine Dakawa ambalo lilikuwa ni maalumu kwa shughuli za kiuchumi! Haya ya Mazimbu ilikuwa ni 1977. So, kama ni Makao Makuu ya kwanza basi huenda ikawa ni hiyo Kongwa na sio Morogoro unless kama Kongwa kwenye maelezo yako iliingia kimakosa.

All in all, kufa kufaana! Madhira ya wenzetu kule Soweto ndiyo yamesababisha kupata Solomon Mahlangu Campus of Sokoine University of Agriculture ambayo zamani (am not sure kwa sasa) ilikuwa inatumiwa na wanafunzi wa SUA wa mwaka wa kwanza na wa pili... kulikuwa na kila kitu including classrooms, dormitories as well as laboratories!
 
Last edited by a moderator:
NasDaz,

..ngoja nitatafuta article niliyoisoma niilete nzima-nzima hapa.

..ila nimewahi kulaumiwa hapa kwa kuleta mi-article mirefu.

..ila kwa uelewa wangu Kongwa ilikuwa ndiyo kambi ya jeshi, na Morogoro ndiyo makao makuu.

..kitu kimoja tulichopatia wa-Tz ni kuwaficha hawa wapigania uhuru mbali kabisa na mijini na wananchi.

..kuwaweka mjini kama Dsm kunge-attract mashambulizi toka kwa makaburu.

..pia wangewekwa karibu na wananchi kungeweza kutokea ugomvi na ukumbuke hawa jamaa walikuwa na silaha za moto.

NB:

..Anna Abdalah alihusika kwa kiasi kikubwa ktk kuwapatia ardhi ya makambi yao wakati akiwa Mkuu wa mkoa. wamemtaja ktk article niliyoisoma zaidi ya mara moja.
 
Last edited by a moderator:
JokaKuu,

Baada ya taarifa yako hapo juu, nami nikalazimika nijishughulishe kidogo. According to mtandao wa South Africa History, it's like ofisi yao ya kwanza (not sure kama ndo tuite HQ) ilikuwa ni Dar es salaam na baadae ndo wakahamishia Morogoro:
In the aftermath of the Sharpeville Massacre, the government banned the ANC and the PAC in South Africa. The ANC then sent Frene Ginwala to Tanzania with instructions to establish an office in Dar-es Salaam, and await further communication. Once in the country, she worked as a journalist while carrying out work for the ANC, which included receiving comrades arriving in Dar-es Saalam. Meanwhile, in 1960 the party instructed Oliver Tambo to clandestinely leave the country and establish offices for the movement in exile. He was also authorised to seek international support for the struggle against apartheid. Tambo skipped the country through Bechuanaland, in a car driven by Ronald Segal. Once in Bechuanaland he contacted Frene Ginwala, who made arrangements for a plane to fly Tambo, Dr Yusuf Dadoo and Segal to Dar-es-Salaam. Upon arrival they were welcomed by Julius Nyerere, and from that time Tanzania became an important point of contact and transit for the ANC in exile.
Lakini linapokuja suala la HQ, pia wanaitaja Morogoro
Despite the initial hesitancy, Tanzania allowed MK to establish camps as transit centres for cadres training in the Soviet Union, China and Czechoslovakia. In 1962 the first military camps were established by Tlou Theophilus Cholo and Joe Modise. The names of the camps were: Kongwa, which held the majority of MK cadres in Tanzania; Morogoro, which functioned as the headquarters of the ANC and MK; and Mbeya and Bagamoyo. Funding and sustenance for the camps came various sources. The OAU Liberation Committee assisted MK by paying for rent and associated expenses for offices in Dar-es-Salaam and Morogoro. In addition the Swedish and Norwegian governments assisted with more funding and technical expertise through various organisations.
Sasa wanakuja kunichanganya wanaposema tena HQ ikawa relocated to Morogoro:
During the 1960s several members of the ANC were deployed in Tanzania. For instance, after JB Marks was elected as Chairman of the SACP at its Fifth Conference held underground in 1962, he was instructed by the National Executive Committee of the ANC to join the headquarters of the External Mission in Tanzania. In 1963 the ANC sent Jo Matlou to Tanzania, where he was followed by his wife Violet Matlou and their children. They became the only complete family living at the Luthuli Camp. Later, in 1965, Ben Turok arrived in Tanzania after serving three years in prison and briefed Tambo on the state of the ANC in South Africa. That same year the ANC relocated its headquarters to Morogoro, but its main military training camp remained Kongwa.
Sharpeville Massacre ilikuwa March 1963. Kutokana na huo mlolongo, kituo chao cha kwanza ANC kilikuwa Dar es salaam ambako waliweka ofisi na kwa kuwa walipofika Dar hawakuwa na ofisi sehemu nyingine, it's obvious ilikuwa considered kama ndio HQ na ndio maana finally wakasema same year (1965) ANC waka-relocate ofis yao to Morogoro na kimsingi, huko Morogoro ndiko ili-operate kwa muda mrefu zaidi kuliko Dar es salaam.

In addition, thanks for this thread coz' hapo kabla, sikupata kufahamu kwamba ANC walimzingua Mwalimu... ama kweli, bora mfadhili mbuzi, utamnywa mchuzi au yale ya shukrani za punda mateke:
In October 1969 Oscar Kombona, a former minister who held the Foreign Affairs, Home Affairs and Defence portfolios in the post-independent Tanzanian government, and others were charged with treason. Kombona was accused of working with the US's Central Intelligence Agency (CIA) to overthrow the government of Tanzania and assassinate Julius Nyerere.

The state's witness was Potlako K Leballo, a founder member of the PAC, which also had camps in Tanzania. Leballo testified that Kombona had tried to enlist him and a co-conspirator. During the trail Leballo alleged that the ANC was also involved in plotting the coup. The Tanzanian government was enraged, and expelled the ANC from Tanzania. All ANC people were to be rounded up and sent to refugee camps, but ANC leaders such as Moses Kotane, JB Marks and Oliver Tambo resisted the move, contending that they were not refuges but freedom fighters. The ANC was forced to close its camps in Tanzania and evacuate its military personnel to the Soviet Union, with assistance from the latter.
http://www.sahistory.org.za/topic/umkhonto-wesizwe-mk-exile?page=8
 
Kuna wenhine walikuwa wapiganaji au wskimbizi wa P.A.C waliishi DAKAWA MOROGORO NA KONGWA DODOMA ila hicho cha huwa hawakitaji taji sijui ni kupoteza historia au nini
 
Titicomb, Bantugbro ,

..huu ni uzi mwingine unaohusu historia ya urafiki wa Tanzania na ANC.

..hapo katikati uliingia dosari ambazo makala niliyonukuu umezielezea.
 
Back
Top Bottom