MOROGORO. Makao Makuu ya Kwanza ya Uhamishoni ya ANC.

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
..katika kupekua-pekua kwenye mtandao nimekutana na kipande cha historia.

..Morogoro ndiyo makao makuu ya kwanza ya ANC uhamishoni.

..hii ni kabla ya ANC kuhamia Lusaka.

..makao makuu ya Umkhonto We Sizwe[ majeshi ya ANC] yalikuwa Kongwa.

..mwaka 1969 kulitokea mfarakano kati ya Tanzania na ANC na kupelekea "kufukuzwa" kutoka Tanzania.

..mfarakano huo ulitokana na tuhuma za ANC kushirikiana na Oscar Kambona kutaka kumpindua Mwalimu Nyerere.

..kutokana na mfarakano huo Tanzania iliwatimua wapiganaji wa ANC, na hivyo kupelekea makao makuu ya ANC kuhamia Lusaka, Zambia.

..kidogo kidogo mahusiano yetu yalirejeshwa ambapo Tanzania ilipokea tena vijana wa ANC kati ya 1972 to 73.

NB:

..kutokana na kupokea kwetu wakimbizi toka kwa ndugu zetu wa Kusini mwa Afrika, Tanzania ilipata kushambuliwa na Makaburu wa Afrika Kusini. Kuna matukio matatu ambayo nimepata kuyasikia. Tukio la kwanza ni shambulizi la manowari za Afrika Kusini zilizoingia Dsm. Tukio la pili ni kuwekwa sumu ktk Mto Ngerengere ambao ulikuwa chanzo cha maji kwenda kwenye kambi la ANC. Tukio la tatu ni jaribio la utekaji nyara wa ndege lililofanywa na kaburu aliyekuwa akifundisha askari wa Umkhonto We Sizwe. Nadhani ilikuwa ni ndege ya Zambia lakini ndege hiyo ililazimika kutua Dsm baada ya vijana wa ANC kumzidi nguvu kaburu huyo na kumkabidhi kwa wanausalama wa Tz.

cc Jasusi, Echolima, EMT, NasDaz, Kichuguu, Shwari, Echolima, Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Ben Saanane, Mohamedi Mtoi, Mag3, MwanaDiwani
 
JokaKuu,
Mbona sielewi? Unasema Morogoro ndio Makao Makuu ya kwanza ya ANC uhamishoni halafu tena unaitaja Kongwa!! Kongwa si upo Dodoma? Morogoro nafahamu ni kweli ANC walikuwa Mazimbu ambayo kwa sasa inatumika kama moja ya kampasi za Sokoine University of Agriculture. Kimsingi, Mazimbu(moja ya Kata za Morogoro Mjini) kilikuwa ni chuo ambacho kilikuwa kinaitwa Solomon Mahlangu Freedom College ambacho kilianzishwa baada ya Soweto Uprising in June 16, 1976' siku ambayo hadi leo inasherehekewa (since 1991) Afrika kama Siku ya Mtoto wa Afrika. Baada ya ile Uprising, wengi walitoroka, na waliokuja Tanzania, hususani vijana (Uprising yenyewe ikihusisha zaidi vijana wanafunzi) ndio waliwekewa chuo pale Mazimbu enzi za Anna Abdallah kama Mkuu wa Mkoa wa Morogoro! Pamoja na Mazimbu, walitengewa eneo lingine Dakawa ambalo lilikuwa ni maalumu kwa shughuli za kiuchumi! Haya ya Mazimbu ilikuwa ni 1977. So, kama ni Makao Makuu ya kwanza basi huenda ikawa ni hiyo Kongwa na sio Morogoro unless kama Kongwa kwenye maelezo yako iliingia kimakosa.

All in all, kufa kufaana! Madhira ya wenzetu kule Soweto ndiyo yamesababisha kupata Solomon Mahlangu Campus of Sokoine University of Agriculture ambayo zamani (am not sure kwa sasa) ilikuwa inatumiwa na wanafunzi wa SUA wa mwaka wa kwanza na wa pili... kulikuwa na kila kitu including classrooms, dormitories as well as laboratories!
 
Last edited by a moderator:
NasDaz,

..ngoja nitatafuta article niliyoisoma niilete nzima-nzima hapa.

..ila nimewahi kulaumiwa hapa kwa kuleta mi-article mirefu.

..ila kwa uelewa wangu Kongwa ilikuwa ndiyo kambi ya jeshi, na Morogoro ndiyo makao makuu.

..kitu kimoja tulichopatia wa-Tz ni kuwaficha hawa wapigania uhuru mbali kabisa na mijini na wananchi.

..kuwaweka mjini kama Dsm kunge-attract mashambulizi toka kwa makaburu.

..pia wangewekwa karibu na wananchi kungeweza kutokea ugomvi na ukumbuke hawa jamaa walikuwa na silaha za moto.

NB:

..Anna Abdalah alihusika kwa kiasi kikubwa ktk kuwapatia ardhi ya makambi yao wakati akiwa Mkuu wa mkoa. wamemtaja ktk article niliyoisoma zaidi ya mara moja.
 
Last edited by a moderator:
JokaKuu,

Baada ya taarifa yako hapo juu, nami nikalazimika nijishughulishe kidogo. According to mtandao wa South Africa History, it's like ofisi yao ya kwanza (not sure kama ndo tuite HQ) ilikuwa ni Dar es salaam na baadae ndo wakahamishia Morogoro: Lakini linapokuja suala la HQ, pia wanaitaja Morogoro Sasa wanakuja kunichanganya wanaposema tena HQ ikawa relocated to Morogoro: Sharpeville Massacre ilikuwa March 1963. Kutokana na huo mlolongo, kituo chao cha kwanza ANC kilikuwa Dar es salaam ambako waliweka ofisi na kwa kuwa walipofika Dar hawakuwa na ofisi sehemu nyingine, it's obvious ilikuwa considered kama ndio HQ na ndio maana finally wakasema same year (1965) ANC waka-relocate ofis yao to Morogoro na kimsingi, huko Morogoro ndiko ili-operate kwa muda mrefu zaidi kuliko Dar es salaam.

In addition, thanks for this thread coz' hapo kabla, sikupata kufahamu kwamba ANC walimzingua Mwalimu... ama kweli, bora mfadhili mbuzi, utamnywa mchuzi au yale ya shukrani za punda mateke: http://www.sahistory.org.za/topic/umkhonto-wesizwe-mk-exile?page=8
 
Kuna wenhine walikuwa wapiganaji au wskimbizi wa P.A.C waliishi DAKAWA MOROGORO NA KONGWA DODOMA ila hicho cha huwa hawakitaji taji sijui ni kupoteza historia au nini
 
Titicomb, Bantugbro ,

..huu ni uzi mwingine unaohusu historia ya urafiki wa Tanzania na ANC.

..hapo katikati uliingia dosari ambazo makala niliyonukuu umezielezea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…