Morogoro: Mama adaiwa kumuua mwanaye kwa kumkatakata na panga

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia Teodora Mkunga (39), mkazi wa Lusange, Kata ya Mtombozi, Wilaya ya Morogoro, kwa tuhuma za kumuua mtoto wake Simon Gervas (8) kwa kumkata sehemu mbalimbali za mwili wake kwa panga.

Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Alex Mkama akizungumza ofisini kwake leo Jumatano Desemba 11, 2024, amesema tukio hilo lilitokea Desemba 8, mwaka huu na chanzo kinadaiwa kuwa matatizo ya akili aliyokuwanayo mwanamke huyo.

"Siku ya tukio, mama huyo alimvamia mtoto wake na kumshambulia kwa kutumia silaha yenye makali sehemu za kichwani na mgongoni, jambo lililosababisha mtoto huyo kupoteza maisha kutokana na kupoteza damu nyingi," amesema Kamanda Mkama.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…