Morogoro: Mbaroni kwa kufungua akaunti ya Corona Facebook na kupotosha Umma

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Mkazi wa Mtaa wa Mazimbu Manispaa ya Morogoro Awadhi Lugoya anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani morogoro kwa tuhuma ya matumizi mabaya ya mitandao kwa kufungua akaunti kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook inayofahamika kwa jina CORONA VIRUS TANZANIA na kutoa taarifa za upotoshaji za ugonjwa wa Corona.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo aprili 4,2020 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro (SACP) Willbroad Mutafungwa amesema mtuhumiwa huyo baada ya kufungua akaunti hiyo amekuwa akitoa taarifa zisizo sahihi na zenye upotoshaji mkubwa kwenye jamii licha ya serikali kutoa onyo kuhusu utoaji wa taarifa za upotoshaji kuhusu ugonjwa huo.

"Mnamo tarehe 1 mwezi aprili mwaka huu majira ya saa 11 jioni jeshi la polisi lilifanikiwa kumkamata kijana mmoja aitwaye Awadhi Lugoya kwa matumizi mabaya ya mtandao wa kijamii ( facebook) kutoa taarifa zisizo rasmi za upotoshaji kuhusu ugonjwa wa corona, mahojiano yanaendelea yakikamilika atafikishwa mahakamani",alisema Kamanda Mutafungwa.

Aidha Kamanda Mutafungwa ametoa tahadhari kwa wakazi wa Morogoro hasa wanaotumia mitandao ya kijamii kuwa makini kuhusu utoaji wa taarifa juu ya ugonjwa wa corona.
 
Hapana. Hii si sawa.

Huyo ni mpuuzi tu anatakiwa kupuuzwa!

Vyombo vya dola viache tabia ya kukimbizana na watu waliorukwa na akili mitandaoni!

Wanatumia nguvu nyingi sana kuhangaika na mambo ambayo sio issues! Tuvitu tudogo tudogo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vizuri watu hawana heshima kwa mamlaka, muda huu atakuwa anajuta kwa ujinga huo
 
Hapana. Hii si sawa.

Huyo ni mpuuzi tu anatakiwa kupuuzwa!

Vyombo vya dola viache tabia ya kukimbizana na watu waliorukwa na akili mitandaoni!

Wanatumia nguvu nyingi sana kuhangaika na mambo ambayo sio issues! Tuvitu tudogo tudogo!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama anakaribia kusitafu atahukumu atafunga watu wengi ili nyota ziongezeke haraka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkazi wa Mtaa wa Mazimbu Manispaa ya Morogoro Awadhi Lugoya anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani morogoro kwa tuhuma ya matumizi mabaya ya mitandao kwa kufungua akaunti kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook inayofahamika kwa jina CORONA VIRUS TANZANIA na kutoa taarifa za upotoshaji za ugonjwa wa Corona.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo aprili 4,2020 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro (SACP) Willbroad Mutafungwa amesema mtuhumiwa huyo baada ya kufungua akaunti hiyo amekuwa akitoa taarifa zisizo sahihi na zenye upotoshaji mkubwa kwenye jamii licha ya serikali kutoa onyo kuhusu utoaji wa taarifa za upotoshaji kuhusu ugonjwa huo.

"Mnamo tarehe 1 mwezi aprili mwaka huu majira ya saa 11 jioni jeshi la polisi lilifanikiwa kumkamata kijana mmoja aitwaye Awadhi Lugoya kwa matumizi mabaya ya mtandao wa kijamii ( facebook) kutoa taarifa zisizo rasmi za upotoshaji kuhusu ugonjwa wa corona, mahojiano yanaendelea yakikamilika atafikishwa mahakamani",alisema Kamanda Mutafungwa.

Aidha Kamanda Mutafungwa ametoa tahadhari kwa wakazi wa Morogoro hasa wanaotumia mitandao ya kijamii kuwa makini kuhusu utoaji wa taarifa juu ya ugonjwa wa corona.
Naunga mkono hoja

Hii ni salama sana kwetu,maana iwapo tutaachiwa kila mmoja aseme lake

Basi hakuna mtu atakaethubutu kutoa Mguu nje(kwa habari za kutishana zisizokuwa na uhalisia wowote)

Naunga Mkono sana juhudi ya Serikali juu ya kudhibiti hili,kwa maslahi mapana ya Taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂.....We will see many this period
 
Back
Top Bottom