Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Aron Daniel (16), mkazi wa mtaa wa Msimamo, Kata ya Kihonda, Manispaa ya Morogoro amekutwa amefariki dunia katika eneo la 'Youth Mission' huku mwili wake ukiwa na majeraha usoni.
Baba mdogo wa marehemu, Baraka Kamele, amesema Aron alikuwa akijihusisha na uchungaji wa mbuzi, ambapo Novemba 16, aliondoka na wanyama hao kwenda machungani, lakini jioni mbuzi hao walirudi nyumbani wenyewe bila mchungaji.
Ameongeza kuwa familia ilianza kumtafuta siku mbili zilizopita na hatimaye jana Novemba 17, mwili wake ulipatikana baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wakazi wa eneo hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, ameithibitisha Mwananchi kutokea kwa tukio hilo, huku akieleza kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha marehemu huenda amefariki kutokana na maradhi ya kawaida.
Soma Pia: Morogoro: Mwanaume mmoja amchoma mwenzake kisu kifuani na kumuua kisa mia 200
“Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina kubaini chanzo halisi cha kifo cha kijana huyo,” amesema Kamanda Mkama.
Aidha katika tukio lingine mwili wa kijana aliyefahamika kwa jina moja la Matabuki mkazi wa Mvalanyaki kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 27-28 umeopolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani humo, baada ya kuzama katika bwawa alipokua akivua samaki.