Morogoro: Msanii Emmanuel Elibariki 'Nay wa Mitego', akamatwa na Polisi

Ungekuwa na msaada kama ungejiuliza kwanini ameimba hivyo alivyoimba, ungesaidia kuzuia wengine wasiimbe tena kuliko hivi vya kuufunika moto kwa blanket na mabua ya mpunga. Tumeamua wenyewe demokrasia itutawale sasa ngoja itawale, tuzuie matusi sio kusemana.
 
Nipo nifungulia sabufa mpaka mwisho, nje ya geti nasikia watoto wanaitikia ile ,chorus " wapo"
 
Samahani mkuu ni lini uliamua kuacha kumuunga mkono Chizi Sizonje.

Ni siku kadhaa nasoma post zako naona umeanza kumdis huyu mtawala mwenye matatizo ya akili.
Sie Tuendeleeni kumjambisha Baba Bashite mpaka akili zimkae sawa!

Wakat alipokuwa Waziri alikuwa haoni tulivyokuwa tunamchana Mkwere mwanzo mwisho? Kwan Yeye Urais wake una tofauti gan na wa Baba Ridh?
 
*NAY WA MITEGO MIKONONI MWA POLISI*

Msanii wa Bongofleva, Nay wa Mitego amekamatwa na Polisi usiku wa kuamkia leo (Machi 26, 2017) mkoani Morogoro.

Habari zinasema kuwa Nay alikamatwa baada ya kumaliza kufanya onyesho lake la muziki na amepelekwa kituo cha Polisi cha Mvomero, Morogoro.
Polisi bado hawajaeleza sababu ya kukamatwa lakini wadadisi wanadai kuwa pengine mashairi ya wimbo wake mpya ndio yatakuwa chanzo cha kukamatwa kwake. [HASHTAG]#WAPO[/HASHTAG]
 
Hii habari hata mimi nimeisikia

Hata hivyo,kwenye ule wimbo hajataja mtu bali amemtaja Bashite wengine hajawataja kwa majina.

Maswali:

Wakimpekeka Mahakamani Bashite aliekashifiwa atakuwa ni nani?Watamsthibitisha vipi Mahakamani?

Anaetajwa katika huu wimbo kuwa hataki kushauriawa atathibitishwa vipi mahakamani kuwa ni fulani ndio amelangwa?

Hamna kesi hapo labda sana sana ni huo wimbo kupigwa marufuku ingawa hata sababu ya kuupiga marufuku itakuwa ni ngumu kuielezea.

Hawa jamaa wanazidi kujijengea uadui na wasanii sijui hata wanawaza nini!!
 
Samahani mkuu ni lini uliamua kuacha kumuunga mkono Chizi Sizonje.

Ni siku kadhaa nasoma post zako naona umeanza kumdis huyu mtawala mwenye matatizo ya akili.

Tafuta Comments za Tangu anaingia na kuanza sakata la Sukari nilimpinga lakini haikunizuia kumuunga Mkono anapopatia!

Hata Kesho akipata kwny Jambo lolote sitosita kumuunga Mkono!

Sina utaratibu wa kumuunga Mkono Mtu kwa kila Jambo Kama ambavyo sina kawaida ya kumkosoa Mtu kwa kila Jambo!

Hata Lowassa huwa namuunga Mkono sana Mtu , mfano alipoweka Siasa pembeni na kuhudhuria Golden Jubilee ya Mkapa ya kutimiza Miaka 50 ya ndoa
 
Safi sana, ashughulikiwe ipasavyo, kucriticise ni haki ila kutukana ni jinai.
Umeusiliza huo wimbo lakini au unakimbilia kuandika tu hajataja jina la mtu amemtaja mheshimiwa unajua hii nchi ina waheshimiwa wangapi unajua maana ya Mheshimiwa........... Au aliposema dokta mtumbua majipu ndio umemuhusisha na naniiihiii kwani madokta wa majipu wapo wengi hata kijijini kwenu yupo .Pia aliyetajwa humo ni Bashite wa kolomije na nikweli ambaye kweli ana jipu ni jirani yangu mbona huku usukumani ukiita watu wenye majina ya Bashite unajaza fuso na majipu ni kawaida kwa mwanadamu yawezekana hata wewe ushawahi kuugua jipu sasa jinai inatoka wapi hakuna kesi hapo sana sana wanampa umaarufu na kumdhalilisha wanaemtetea mwisho wa siku anashinda kesi labda BASATA ndio wamfungie kufanya mziki maisha au miaka kadhaa kutegemeana na sheria zao ila jinai hakuna hapo!!! Elimu Elimu Elimu............
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…