Morogoro: Mwanaume mmoja amchoma mwenzake kisu kifuani na kumuua kisa mia 200

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamzuilia Kulwa Bosco, anayejulikana kwa jina maarufu la Rasta, ambaye ni mfugaji mkazi wa Kijiji cha Sinyaulime, Tarafa ya Ngerengere, wilayani Morogoro, kwa tuhuma za mauaji.

Inadaiwa kuwa alimuua Hussein Nyabu (35) kwa kumchoma kisu kifuani, kitendo kilichosababisha kifo cha marehemu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Alex Mkama, ameeleza kuwa chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliotokea wakati Kulwa na Hussein walipokuwa wakibishana kuhusu kiasi cha Tsh. 200 walichokuwa wakigombea walipokuwa wakicheza pool table.

Ndipo, Kulwa akaamua kutoa kisu na kumchoma Hussein, na kusababisha kifo chake.

Tukio hilo limetokea September 29,2024 saa 1 jioni katika Kitongoji cha Ngerengere Kaskazini Kata ya Ngerengere Wilaya ya Morogoro vijijini wenye baa ya Itonyange maarufu kama Maokoto, upelelezi wa awali umebaini chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi uliosababishwa na kubishania Tsh. 200 wakiwa katika mchezo wa kamari ya po table ndipo Mtuhumiwa alitoa kisu na kumchoma marehemu”

Kamanda huyo wa Polisi aliongeza kwa kusema:

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linatoa wito kwa Wananchi hususani Vijana kuacha kujichukulia sheria mkononi lakini pia wajikite kwenye kufanya kazi ili kujiingiza kipato cha halali na sio kutegemea kamari

Source: Millard Ayo
 
Janga la ukosefu wa ajira linawaangamiza Sana vijana siku hizi.
 
Tatizo la afya ya akili.
 
Ni mia 2 au

mia 200​

 
Roho ya mauaji iliyopo ndani ya mkuu ndo inayotendakazi ndani ya nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…