Morogoro: Mwanaume wa miaka 46 ajinyonga kwa kutumia chandarua, alikuwa na changamoto afya ya akili

Morogoro: Mwanaume wa miaka 46 ajinyonga kwa kutumia chandarua, alikuwa na changamoto afya ya akili

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Emilian Makalla (46) Mkazi wa Bigwa Barabarani wilaya ya Bigwa Mkoani Morogoro amejinyonga kwa kutumia chandarua na kufariki dunia nyumbai kwake huku chanzo kikiwa hakijafahamika.

Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu wameeleza kwamba Emillian alikuwa akisumbuliwa na changamoto ya ugonjwa wa afya ya akili jambo ambalo lilikuwa likipelekea kupelekwa hospitali mara kwa mara japo kwa sasa hakijulikani chanzo kulichopelekea kufanya maamuzi ya kujinyonga.

“Kaka yetu alikuwa na matatizo ya akili mara nyingi ana anguka na kufingwa mikono na miguu tunapigiwa simu tunahangaika nae anapona anarudi vizuri na kazi yake ni kulima na kufyatua matofali” Amesema Stella Thomas dada wa marehemu.

Soma Pia: Mwanafunzi darasa la saba ajinyonga kwa kutumia kamba ya chandarua

Aidha Afisa Mtendaji Kata hiyo amefika eneo la tukio na amesema tayari mwili wa marehemu umechukuliwa na kupelekwa hospitali na uchunguzi unaendelea kujua hasa nini kilipelekea Emilian kufanya maamuzi hayo
 
Bigwa barabarani ndio sehem gani? Na toka lini bigwa imekuwa wilaya?
 
Back
Top Bottom