Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mwenyekiti wa Mtaa wa Makaburi A, Kata ya Mji Mpya, Manispaa ya Morogoro kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Hamis Lukinga maarufu kama 'Mzee Kiuno' (70) aliyehudumu kwenye uongozi huo kwa miaka 30 sawa na vipindi sita amechaguliwa tena kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano.
Akizungumza na Mwananchi Digital Lukinga amesema kwa mara ya kwanza aliingia madarakani mwaka 1994 ukiwa ni uchaguzi wa kwanza uliohusisha mfumo wa vyama vingi na tangu hapo aliendelea kuchaguliwa ndani ya chama hadi kwa wananchi wa mtaa huo.
Soma Pia: Morogoro: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024
Lukinga ametaja moja ya siri za ushindi wake ni uchapakazi unaowafanya wananchi wamkubali lakini pia uwazi kuwa kusaidia na kushirikiana na wananchi wake katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo.