Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
TAARIFA KWA UMMA Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linachunguza tukio la kifo cha Yosia Johani Keya (25) mwanachuo mwaka wa tatu katika chuo Cha kilimo cha Sokoine (SUA).
Tukio hilo limefahamika tarehe 9.3.2025 asubuhi huko katika eneo la makazi ya wanachuo hao kampasi ya Mazimbu, kata ya Mazimbu, Manispaa ya Morogoro.
Marehemu amekutwa amekufa kwa kujinyonga kwa kutumia shuka ambalo alifunga kwenye Kenchi la makazi ya wanachuo upande wa baraza la nyuma. Uchunguzi wa tukio hilo umeanza ili kubaini chanzo cha tukio hilo.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa vijana na watu wengine kuacha kuchukua maamuzi kam hayo ya kujitoa uhai kama suluhu ya changamoto zao.
Badala yake watumie fursa ya madawati mbalimbali ya ushauri nasaha na nasihi kueleza changamoto hizo. Imetolewa na; Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro.
Imetolewa na;
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro