Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limemkamata Subira John (25) mkulima Mkazi Mtendeni kwa kosa la kutelekeza kichanga.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa Morogoro, SACP Alex Mkama tukio hilo limetokea Novemba 8, 2024 majira ya mchana katika eneo la K Park bar kitongoji cha Mbumi Kata ya Mbumi Wilaya ya Kilosa ambapo mtuhumiwa huyo alikifukia kichanga hicho chenye umri wa siku moja jinsia ya kiume na kuacha kichwa nje ya shimo na kutoroka kusikojulikana.
Ikumbukwe kuwa Novemba 8, 2024 kupitia mitandao ya kijamii zilisambaa taarifa za utelekezwaji wa kichanga hicho na Jeshi la Polisi lilianza uchunguzi ili kubaini mtuhumiwa wa tukio hilo, baada ya ufuatiliaji Disemba 2, 2024 mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa kajificha kwenye nyumba ya wageni isiyo na jina maarufu (Gesti bubu)
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na taasisi nyingine ikiwemo Ustawi wa jamii lilifanikiwa kukichukua kuchanga hicho na kukipeleka katika kituo cha kulelea watoto Mgolole kilichopo kata ya Bigwa na kwasasa kichanga hicho kinaendelea vizuri huku upelelezi ukiendelea kukamilishwa kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria.
Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kutelekeza vichanga na badala yake wavilee kwani hilo ni