Morogoro tunauziwa vifaa vya maji bei juu. Yaidaiwa ni maelekezo ya Wizara

Morogoro tunauziwa vifaa vya maji bei juu. Yaidaiwa ni maelekezo ya Wizara

Faana

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
38,657
Reaction score
44,759
Jana nilikwenda ofisi ya MORUWASA - Morogoro kufuatilia maombi yangu ya kuunganishiwa maji nyumbani kwangu, niliandikiwa invoice kuwa natakiwa kulipa zaidi ya Tsh 300,000 kwa umbali usiozidi mita 8 toka lilipo bomba (wao wanaita tawi) la mamlaka hiyo ambapo wengi wamechukulia hapo.

Nikawauliza mbona bei ipo juu kiasi hicho? nikaambiwa gharama za vifaa zipo juu, nikaenda dukani mjini kuuliza bei za vifaa, nilichoshangazwa ni kwamba vifaa hivyohivyo vinauzwa kwa nusu ya bei, kwa mfano seal tape inauzwa Tsh 500 dukani, lakini wao MORUWASA wanauza Tsh 900.

Nikarudi MORUWASA na kumuuliza mfanyakazi mmoja wa Mamlaka hiyo kwanini mnatuuzia vifaa kwa bei mara mbili ya ile ya madukani, na vifaa ni vilevile na inasemekana Mamlaka inachukua kwa wauzaji haohao wa mjini si kwamba mnaagiza toka kiwandani Dra es Salaam. Mfanyakazi yule akasema ni maagizo kutoka juu, na juu ni huko Wizarani kwako Waziri wa maji.

Swali:
  • Kwanini Waziri unatumia Mamlaka za maji kutunyonya wananchi?
  • Kwanini unaiagiza Mamlaka ya maji kutulazimisha wananchi kununua vifaa vya kuunganishia maji kwao wakati tunafahamu Mamlaka ina jukumu la kutuunganishia maji na siyo kutuuzia vifaa?
  • Sawa yawezekana kuna sababu ya msingi kufanya hivyo, lakini kwanini mnaweka middlemen wa kutuuzia vifaa kwa bei mara mbili tofauti na madukani?
  • Lengo lako ni nini kutuibia wananchi tena waziwazi?
  • Je umetumwa na Rais kuongeza mapato kwa kutuibia?
Hii siyo sawa hata kidogo, fedha ya dhuruma haina baraka ndugu Waziri, tunaomba uwatumikie wananchi kwa haki, maagizo yako kwa hizi mamlaka kutulazimisha kununua vifaa vya maji na wakati huohuo kutupandishia bei na kutukatalia kuunganishiwa maji iwapo tutakuwa hatujanunua vifaa vyako, ni ukiukwaji wa haki zetu raia, hii inatufanya tuamini kuwa bei hizi zimewekwa ili ninyi viongozi mnufaike na makusanyo hayo, kuna tetesi kwamba huwa mnawapigia simu wakurugenzi wa mamlaka hizo kuwaomba fedha kwa mambo binafsi, sasa tunaanza kuamini kwamba mnatuhujumu wananchi ili kupata fedha haramu inayopatikana kwa dhuruma.

Nawasilisha
 
Ungeweka na hiyo invoice hapo kama ushahidi. Kuna mashirika ya umma ovyooo sana kama hiyo moruwasa maji yenyewe shida.
 
HAO moruwasa AKILI hawana.

Kwani NI wasiagize vifaa kutoka viwandani na magari ya kubebea wanayo.
 
ungeweka na hiyo invoice hapo kama ushahidi. Kuna mashirika ya umma ovyooo sana kama hiyo moruwasa maji yenyewe shida.
Mkuu nilipata hasira sana kuona nalazimishwa kuibiwa tena na serikali, hiyo invoice hata sijui niliitupa wapi.
 
Wewe lipa bhana, changia maendeleo ya nchi si unajua km nchi tuna mipango mingi?
 
Vifaa vya bomba NI bei rahisi sanaa.na vina hela kinoma ukiwa sehemu nzuri
Ni kweli Mkuu, lakini hali si hiyo hapa mjini, wenzetu wanatumia hiyo kama namna ya kujineemesha wao na hao viongozi wa juu
 
Sisi wakazi wa kingolwira majengo mapya (mtaa wa bomba la mafuta).

Kuna miundo mbinu ya maji iliwekwa zamani na miradi ya Mh Mariam ditopile ambayo ilifika kwetu na maji tulikuwa tunapata vizuri tu hadi april mwaka jana 2021.(sisi tunaamini before JPM passing).

Yalitoka vizuri iwe mvua liwe jua.ila kwa sasa hatupati maji .

Toka august mita zetu hazisomi maji tunauziwa na bowser kwa sh 20000 kwa lt 1000 kwa vile huku ni mbali.(inatugharimu).

Mwanzo tuliambiwa ni ukame, mvua imenyesha tunaambiwa ni matope,

Ajabu ni taasisi za karibu tunaotumia mradi hii ya karibu karibu yaani maeneo ya chem chem ya mlima yaani magereza, jeshi na mkambarani hadi mikese wao hawakuwa na kadhia hii, Jeshi la pangawe wanauza masaa 24 mabomba 4 na utokaji ni presha nzuri sana.ajabu sisi tulio chini ya mlima wa jeshi hatupati ni IMANI pamefungwa mahali kututaabisha.

Sisi tunaambiwa ufumbuzi ni kuusubiria mradi wa mwindu, mazimbu, lukobe, yepsa , tungi na kingolwira ufike.

Tunachokiona moja SSH anahujumiwa.watu kauli zao ni kabla yalitoka ila baada ya kutenguliwa mkurugenzi wa moruwasa hatupati maji.

Pili, Diwani ni magumashi ni mbabe na watu tunamuogopa.
Tatu mkuu wa wilaya amekagua sana vyanzo vya maji lakini waliandaa mabomba na kumwambia wanabadili mradi wa zamani kwenye ule mradi aliowahi simamia Ditopile.

Sasa mvua zinanyesha hatujapata hata tone na ni wiki ya pili mvua zinanyesha.
 
Back
Top Bottom