SAUTIYANGU
New Member
- Oct 23, 2024
- 4
- 2
Mimi Mkazi wa Mindu, Manispaa ya Morogoro jamani huku kwetu kuna kero ya maji mno licha ya kuwepo kwa bwawa lakini sisi hatuna huduma ya maji mpaka imekuwa kero inatulazimu kutumia maji ya kwenye Visima na Makorongo hali ambayo ni hatari kwa Afya zetu na ni hatari kupata magojwa ya milipuko.
Kwa sasa hivi mvua hazipo hata hayo maji ya korongoni hatuyapati tunalazimika kununua maji ya chumvi na hayo ya chumvi yanauzwa ndoo shilingi 100.
Umeme usipokuwepo hatuyapati kabisa mpaka inatulazimu kwenda kuyafata hukohuko bwawani kitu ambacho si salama pia hata kwa wenzetu ambao wanapata huduma ya maji kupitia bwawa hilo.
Mamlaka husika ya maji Morogoro (MORUWASA) mko wapi? tunaomba Serikali itusaidie tunasikia tu, kuna mradi na mabomba yataanza kuwekwa lakini hatuyaoni ahadi imekuwa mwezi ujao tutaanza kusambaza mabomba lakini hatuyaoni.
Asilimia kubwa wanaoteseka ni wakina Mama na watoto kudamka alfajiri saa kumi na moja kwenda kufuata huduma ya maji ni hatari.
Mbunge wa Jimbo letu AbdulAziz Abood tunaomba uliangalie hili wananchi na wakazi wa mindu tupate huduma ya maji.’
Kuna Watoto wengi hawaendi shule, muda wanaotakiwa kuwa shuleni wao wanakuwa bize kutafuta maji.
Mbali na hapo kuna mazingira hatarishi ya Watoto na Wanawake wanaoenda kutafuta maji majira ya alfajiri na wengine usiku.
Kwa ufupi hali ya ukosefu wa maji imekuwa janga linaloumiza watu wengi, viongozi wa Kisiasa wamekuwa wakitoa ahadi ambazo hazikamiliki.
Wananchi tunateseka, tunaomba ujumbe huu umfikie Rais Samia na viongozi wote wa juu wajue kuwa sisi pia ni Wananchi wao nani wapiga kura wao.