Morogoro: Watuhumiwa Watano wa makosa ya mauaji Wilayani Kilosa wakamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi

Morogoro: Watuhumiwa Watano wa makosa ya mauaji Wilayani Kilosa wakamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Moro 1.jpg

Moro1.jpg
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linaendelea kuimarisha operesheni zake dhidi ya uhalifu na wahalifu. Operesheni hizo zimepata mafanikio makubwa ikiwemo kuwakamata watuhumiwa watano wa matukio ya mauaji ambayo yametokea katika wilaya ya Kilombero na Kilosa kati ya Mei 26, 2024 na Juni 2, 2024.

Miongoni mwa watuhumiwa hao ni Erick Maguru Julias (33) mkulima, mkazi wa Miembeni. Alikamatwa Juni 2, 2024 baada ya kutuhumiwa kumuua kwa kutenganisha kichwa na kiwiliwili mtoto wake wa kufikia aitwae Johnson Eniath Ngonyani (6) mwanafunzi wa shule ya awali Mwembeni Mlimba. Mtuhumiwa alimuua mtoto huyo na kumnyofoa baadhi ya viungo ambavyo ni kichwa, viungo vya uzazi na kukata viganja vyote viwili, tukio ambalo lilitokea Juni 1, 2024 usiku katika kitongoji cha Kigamboni, Kijiji cha Mwembeni, Kata ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero, Mkoa wa Morogoro. Baada ya tukio hilo mtuhumiwa alikamatwa kutokana na taarifa za raia wema ambapo alihojiwa na kukiri kufanya mauaji hayo na kutoa ushirikiano wa kuonyesha sehemu alikoficha hivyo viungo.

Wakati huo huo Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro limemkamata Jovina Stephen Mwakiyee, (33), mkulima na mkazi wa Kijiji cha Mang'ula A kwa tuhuma za kula njama na kumuua mume wake wa ndoa. Tukio hilo limetokea Juni 1, 2024 usiku huko katika kitongoji cha Gengeni, Kijiji cha Mang'ula A, kata ya Mang'ula, wilaya ya Kilombero, Mkoa wa Morogoro, ambapo mwalimu aitwae Christian Revocatus Tungaraza (39) mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Signal aliuwawa kwa kupigwa na kitu butu wakati akiwa amelala ndani ya nyumba yake. Upelelezi zaidi unaendelea kuwakamata watuhumiwa wengine walioshiriki mauaji hayo.

Aidha, Katika operesheni hiyo Jeshi la Polisi Morogoro limefanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa, wanne ambao ni Hassan Mohamed Mbwambo (31) mganga wa kienyeji, mkazi wa Same, Mkoa wa Kilimanjaro, John Samwel Matunda (20) Bodaboda, mkazi wa Dumila wilaya ya Kilosa, Boniface Welesi Mwendi (31) Mkulima, mkazi wa Dumbalume Berega na Neema Johnson Mbwambo (32) Mkulima, mkazi wa Moshi.

Watuhumiwa walikuwa wanatafutwa kwa mauaji ya mfanyabiashara aliyefahamika kwa majina ya Elly Kimaro (Elly Maro) (53) mfanyabiashara wa madini, mkazi wa jijini Arusha, Tukio ambalo lilibainika Mei 26, 2024 saa mbili kamili usiku. Watuhumiwa baada ya kumuua walimnyang'anya kiasi cha shulingi milioni 15.

Kabla ya tukio hilo Mei 25, 2024 Marehemu alisafiri kwa basi liitwalo Mapenzi ya Mungu akifuatana na Hassan Mohamed Mbwambo kuja Mkoa wa Morogoro eneo la Turiani kwa ajili ya kufanya biashara ya madini.

Baada ya kufika Eneo la Turiani Mtuhumiwa kwa kushirikiana na John Samwel Matunda akiwa na pikipiki Walimteka hadi Kijiji cha Berege na kumnyang'anya kiasi hicho cha pesa na kumtaka mume wa marehemu awatumie kiasi kingine cha Tsh.milioni 5 ili aweze kuachiwa. Baada ya kupatiwa kiasi hicho walimuua na kumtelekeza katika shamba la Mbaazi katika Kijiji cha Berega hadi alipoonekana na wasamalia wema.

Kwa upande mwingine, Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linafuatilia malalamiko ya ndugu Wolter Fuime (32) mkazi wa Mjimwema ambaye analalamika kushambuliwa na askari Polisi waliokuwa doria. Mei 26, 2024 askari Polisi walifika kwenye banda lake la kuonyesha video majira ya usiku kufanyia kazi taarifa fiche kuwa eneo hilo linatumiwa kufanya matendo yaliyo kinyume na maadili ikiwemo kuonyesha picha za video zisizo na maadili kwa Watoto na kumkamata mmiliki huyo wa banda na baadae kumwachia kwa dhamana.

Baadae alilalamika kuwa hajisikii vizuri hivyo anaomba hati ya kutibiwa ambayo amepewa na kwa kuwa kila hati ya matibabu inayotolewa lazima kuwe na uchunguzi, hivyo tumechukua hatua ya kulichunguza suala hilo kubaini ukweli.

Uchunguzi wa matukio haya unakamilishwa haraka iwezekanavyo kwa ajili ya maamuzi mengineyo kwa mujibu wa sheria.

Nitoe wito kwa wananchi kuchukua tahadhari mbalimbali dhidi ya wenza wao katika Maisha. Matukio haya yamesababishwa na sababu kadha wa kadha ikiwemo Imani za kishirikina, Tamaa ya mali na migogoro ya kifamilia. Jamii ichukue jukumu lake la msingi la kusimamia maadili ya watu wake ili kuepukana na matukio haya mabaya ya ukatili. Jeshi la Polisi kwa mara nyingine linawashukuru sana wananchi ambao wamesaidia kwa kubadilishana taarifa na kufankiwa kuwakamata watuhumiwa.

Imetolewa na
Alex Mkama-SACP
Kamanda wa Polisi Mkoa Morogoro.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia, Erick Julias (39) mkazi wa Mlimba wilayani Kilombero kwa tuhuma za kumuua na kumtenganisha kichwa pamoja na viungo vingine mtoto wake wa kufikia, Johnson Ngonyani (6).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 4, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema pamoja na mtuhumiwa huyo kumkata kichwa, pia alimkata seheme za siri (uume na korodani) na viganja vyote viwili.

Kamanda Mkama amesema mtuhumiwa alitenda ukatili huo Juni 1 mwaka huu majira ya usiku katika Kitongoji cha Kigamboni, Kijiji cha Mwembeni, Mlimba Wilaya ya Kilombero.

Amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa kutokana na taarifa za raia wema na baada ya kuhojiwa Polisi amekiri kufanya mauaji hayo na ametoa ushirikiano kwa kuonyesha sehemu alikoficha viungo hivyo.

Mwingine amuua mumewe

Wakati huohuo, Polisi wamemkamata Jovina Mwakiyee (33) mkazi wa Kijiji cha Mang'ula A kwa tuhuma za kula njama na kumuua mume wake Christian Tungaraza (39), mwalimu mkuu Shule ya Msingi Signal.

"Tukio hili limetokea Juni 1, mwaka huu majira ya usiku huko katika Kitongoji cha Gendeni, Kijiji cha Mang'ula A, Wilaya ya Kilombero ambapo mtuhumiwa huyo amedaiwa kula njama zilizofanikisha kuuawa kwa mumewe," amesema Kamanda Mkama.

Mkama amesema mwalimu huyo akiwa amelala na mtuhumiwa (mke wake) na watoto wao wawili, alivamiwa ndani na kuuawa kwa kupigwa na kitu butu kichwani.

Amesema polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuwapata watuhumiwa wengine wanaodaiwa kushirikiana na mwanamke huyo.

Katika tukio jingine la mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Elly Kimaro (53) mkazi wa Arusha, Polisi wamewakamatwa Hassan Mbwambo (31), mganga wa kienyeji mkazi wa wilayani Same, Kilimanjaro na John Matunda (20), dereva wa bodaboda mkazi wa Dumila Wilaya ya Kilosa.

Wengine ni Boniface Mwendi (31), mkazi wa Kijiji cha Berega na Neema Mbwambo (32) mkazi wa Wilaya ya Moshi vijijini.

Kamanda Mkama amesema tukio hilo la mauaji ya mfanyabiashara huyo lilitokea Mei 26, 2024 saa mbili usiku, ambapo watuhumiwa wanadaiwa kumnyang’anya marehemu Sh20 milioni na kisha kumuua.

Kamanda Mkama amesema Kimaro alisafiri kutoka Arusha hadi Turiani mkoani Morogoro kufanya biashara ya madini akiwa na Hassan Mbwambo ambaye ni mmoja wa watuhumiwa.

"Baada ya kufika eneo la Turiani mtuhumiwa kwa kushirikiana na mwenzake Samwel Matunda wakiwa na pikipiki, walimteka hadi Kijiji cha Berega na kumyang'anyana fedha na kumtaka mume wa marehemu aongeze Sh5 milioni ili wamuachie mkewe," amesema Kamanda Mkama.

Alisema baada ya kupatiwa kiasi hicho cha fedha, walimuua mke na kuutelekeza mwili wake katika shamba la mbaazi hadi mwili huyo ulipoonekana na wasamaria wema.

Kufuatia matukio hayo ya mauaji hayo, Kamanda Mkama amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya wenza wao, kwani matukio mengi ya mauaji yamehusisha mapenzi, imani za kishirikina, tamaa ya mali na fedha pamoja na migogoro ya kifamilia.

Chanzo: Mwananchi
 
Umeshindwa kuandika hata kucopy na kupaste huwezi
 
Asante kwa taarifa nzuri, Hiyo habari ya mwalimu Christian kuuwawa kwa njama za mke wake imeugusa sana Moyo wangu [emoji24][emoji24]
 
Back
Top Bottom