Evarm
JF-Expert Member
- Aug 30, 2010
- 1,994
- 1,540
Habari zenu wakuu,
Idara ya maji safi Morogoro mjini (MORUWASA) mnatutesa sana wakazi wa kiegea A na B. Mmetuunganishia haya mabomba lakini hamtaki kutufungulia maji. Mfano leo hii ni zamu yetu ya maji lakini mmefungulia kidogo sana yaani tumekinga ndoo tano tu mmekata. Hizi ndoo tano kwa familia ni maji kidogo sana kwa wiki nzima. Angalau mngekuwa mnafungulia siku nzima tungewaelewa halafu hata speed ya maji ni ndogo mno.
Tunatoa tahadhari kwa mfungua maji (Tunakufahamu), na uongozi mzima wa idara ya maji MORUWASA. Safari ijayo tutakuja huko huko ofisini tuonane na viongozi wenu maana huu sio uungwana. Kama kuna shida muwe mnatuambia mapema au mnataka kutuuuzia maji kwenye hayo maboza yenu? Natumaini hili angalizo mtalifanyia kazi hizi sio kama zama zile...
Wasalaamu,