Moses Phiri asingemuweka Fiston Mayele Kichwani mwake haya Majeraha asingeyapata

hii mbona kama promo kwa Mayele na dongo kwa Phiri na mbumbumbu fc wote , dizaini kama vile Genta kavaa uzi wa wananchi!! Au kahamia jangwani coz msimbazi hapasomeki na Barabara katimka?
Msichokijua wengi hapa JamiiForums ni kwamba licha ya Mimi kuwa mwana Simba SC ila pia ni Mwanamichezo hasa, Nimeshacheza Mpira wenyewe na pia ni Mchambuzi wa Soka la Bongo ninayepatikana tu hapa Mtandaoni JamiiForums.

Namheshimu na Nampenda mno tu Mshambuliaji wangu Moses Phiri ( General ) ila Navutiwa zaidi Ufungaji Magoli wa Kibabe na wa Kiupambanaji alionao Fiston Mayele ( Predator ) wa Yanga SC.

Mayele anafunga kwa Kuibeba Yanga SC yake ila Moses Phiri anafunga kwa Kushindana na Mayele na Kujipaisha Yeye Mwenyewe na Matokeo ya Ushindi kwa Simba SC Kwake huja mwisho.

Nikiwa kama Critical Observer angalieni Mayele asipofunga Goli na akifunga mwingine bado Body Language yake utaiona ana Furaha na hana Kinyongo kwa aliyefunga.

Rejeeni Video ya Mechi ya Geita Gold FC na Simba SC pale CCM Kirumba Mwanza. Kila walipofunga Wengine ( na siyo Yeye Phiri ) utaona hata tu Ushangiliaji wake na Wenzake pamoja na Tabasamu lake ni la Kinafiki na Kujilazimisha ili asishtukiwe.

Mshambuliaji Moses Phiri kwa jinsi Mabeki wa Kagera Sugar FC walivyokuwa Wakifika Kwake mazima na Kugongana nae kama angejiongeza Kiakili ilikuwa ni Kengele tosha Kwake kuwa kulikuwa na Mission ya Kumuumiza hivyo angebadili upesi Style of Play and Striking ili wasifanikiwe badala yake nae kwa kutaka Sifa huku Kichwani mwake akiwa Kambeba Fiston Mayele akawa anataka Kulazimisha kupita katika Msitu wa Mabeki Katili na hatimaye kujikuta anaumizwa vibaya vile.

Akipona ajirekebishe hi ndiyo Bongo.
 
Sasa hapo ndio UNAKOSEA KUSEMA mabeki wenye DNA za yanga wakati hao mabeki wanacheza Kwa ajili ya timu yao
 
Kwa hiyo hutaki Phiri aipambanie timu, kufunga magoli na kuipigania timu zote ni kazi zake, hapa suala sio kumuwaza Mayele wala yeyote mwingine.
 
Hili unalosema lilionekana wazi mechi ya Geita Gold.
 
Ile ni ajali tu kama ajali nyingine kwani ISRAEL MWENDA yeye alimuweka nani kichwani?mbona mpaka muda huu anauguza majeraha,acha kufikiria kindezi
 
Mayele anawatesa wengi..!!! Kuanzia wachezaji mpaka mashabiki wa Makolo a.k.a ngada FC
 
Kwa hiyo asifunge kwa vile mayele anafunga?
Aliyemweka mwenzie kichwani ni nani kama si mayele?
Hivi umeona rafu anazochezewa?Au unataka asiguse kabisa mpira?
Ujuaji mwingine ni wa kipuuzi

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…