Kama kuna jambo limevuruga ustawi wa Simba msimu huu ilikuwa ni majeraha ya Moses Phiri. Ilichukua muda Simba kujijenga bila uwepo wake ukichukulia tayari alikuwa tegemeo la kwanza katika timu katika ufungaji wa magoli.
Baada ya kupona, Simba walikuwa wavumilivu sana katika kumrudisha kikosini hadi wengine tukawa tunahoji niaje. Kweli mambo mazuri yanahitaji uvumilivu. Naamini Moses Phiri yuko gado sasa kuipambania Simba 100%.
Toka amerudi hajafunga goli ila ametoa assist muhimu na za kutosha na mashuti yake mengi yalikuwa on target.