Moshi: DC apiga marufuku watu kusafiri bila kuvaa barakoa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mkuu wa wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro Said Mtanda Julai 19.2021 amezitaka mamlaka za usafirishaji kuzuia magari kuondoka stendi ikiwa abiria wake hawaja vaa barakoa kujikinga na virusi vya Corona.

Nimekuja kuwaambia ukweli na Rais na Serikali yake wamesha sema Corona ipo tena wimbi la tatu ni hatari zaidi Wafanyabiashara masokoni chukueni tahadhari na hakikisheni kila mtu amevaa barako hii ni kwa faida ya wote kuwa salama" DC Moshi, Mtanda

"Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani simamieni jambo hili ikiwa mtu hajavaa barako gari isiondoke na Askari asiye simamia agizo hili atachukuliwa hatua kali kwa sababu tukiweka mchezo katika janga hili tutaangamia"Said Mtanda, DC Moshi
 
hamtaki tufe ili muendelee kupata kodi ya mshikamano au kwa sababu mnatujali?
 
Ni upotevu wa Mali, akili na Muda kwa kuhangaika na vijimafua visivyoweza kuua hata kifaranga cha kuku
 
Dah , hata huku Chugga Jana na leo nimepokea taarifa ya misiba mitano ya wafiwa nao fahamiana nao . This sh** is real
 
Kwani yule Meya aliyewatoa nje waliovaa barakoa kwenye kikao cha madiwani anasemaje?
 
Waganga wa kienyeji hawana msaada kwenye hilo mheshimiwa DC?
 
Hapa ndipo utaona namna mtu anakosa ubunifu yaana anapewa nafasi asiyoimudu.
 
Yani utasema siyo huko ambako kuna mheshimiwa aliwatoa wenzake kikaoni kisa hawajavaa barakoa. Aisee!
 
Hizo barakoa watazipata wapi na michango ya corona iliyochangwa ilikwendaga wapi
 
Nitavaa barakoa siku nikiprove kuwa waliokufa
Huko ulaya wanavaa sana barakoa, lkn cha ajabu Corona inapita nao tu yaani wanakufa kama kuku 😳

Sasa kwetu tulazimishane kuvaa hiyo mibarakoa ili iweje, kama kufa tutakufa tu.

DC hana ideas mpya, anyamaze tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…