Mgambo maarufu katika kata ya Bomambuzi Manipaa ya Moshi aliyekuwa pia dereva bajaji, Farjala Abdallah ameuawa na watu wasiojulikana, huku Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro likiahidi kuwasaka kwa udi na uvumba waliofanya mauaji hayo.
Mwili wa marehemu ulipatikana leo alfajiri ya Februari 21,2024 katika eneo la Uwanja wa Mandela ukiwa na majeraha, huku majirani wakifichua kile walichokisikia usiku wa manane kuwa marehemu alikuwa akijitetea kuwa sio mwizi.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Moshi, Azizi Kalokola ,Diwani wa Kata ya Bomambuzi, Juma Raibu na mashuhuda mbalimbali wameelezea namna walivyopata taarifa za kuonekana kwa mwili wa dereva huyo leo alfajiri. Huku Diwani Raibu akiahidi kutoa kitita cha Sh500,000 kwa mtu atakayetoa taarifa fiche na sahihi zitakazosaidia kukamatwa kwa watu waliofanya mauaji hayo.
apumzike kwa amani mgambo....
lakini kwenye mkoa wetu ule migambo wanazulumu sana haki za watu kulingana na sheria ndogo ndogo zilizowekwa na mamlaka ya miji mfano wilaya ya mwanga migambo wengi waliokua wakizulumu wamama wa samaki au wafugaji wameishia kulogwa kuwa vichaa na wengine kukosa uelekeo wa maisha kwakua walidhulumu mali za watu wapo waliodiriki kupiga wazee na ikawa mwisho wao...
tukio la mauaji ni unyama uliopitiliza ila wanatakiwa wajifunze kuna sehemu wanakosea sana na hawatakagi kujiongeza mifano ya wenzao wanayo ila wanapotekeleza majukumu yao wao ndio huonekana wabaya ..
imagine unamzulumu MPARE mtu ambaye kesi ya kuku anauza ng'ombe ili apate haki...
Moshi na Arusha hizi kesi ni kama zinafanana,
Hapo ukute jamaa alikuwa kiherehere cha kuwachomesha wauza
mirungi, bangi, na gongo sasa wajumbe wakamkalia kamati ya majukumu ya Izrail
Wakapita nae.
Mgambo maarufu katika kata ya Bomambuzi Manipaa ya Moshi aliyekuwa pia dereva bajaji, Farjala Abdallah ameuawa na watu wasiojulikana, huku Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro likiahidi kuwasaka kwa udi na uvumba waliofanya mauaji hayo.
Mwili wa marehemu ulipatikana leo alfajiri ya Februari 21,2024 katika eneo la Uwanja wa Mandela ukiwa na majeraha, huku majirani wakifichua kile walichokisikia usiku wa manane kuwa marehemu alikuwa akijitetea kuwa sio mwizi.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Moshi, Azizi Kalokola ,Diwani wa Kata ya Bomambuzi, Juma Raibu na mashuhuda mbalimbali wameelezea namna walivyopata taarifa za kuonekana kwa mwili wa dereva huyo leo alfajiri. Huku Diwani Raibu akiahidi kutoa kitita cha Sh500,000 kwa mtu atakayetoa taarifa fiche na sahihi zitakazosaidia kukamatwa kwa watu waliofanya mauaji hayo. View attachment 2911043