Pre GE2025 Moshi Mjini pamoto, kada CCM atumia jina la Rais kujinadi

Pre GE2025 Moshi Mjini pamoto, kada CCM atumia jina la Rais kujinadi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Joined
Oct 17, 2024
Posts
6
Reaction score
7
Hali ya kisiasa katika jimbo la Moshi mjini inazidi kupamba moto kuelekea uchaguzi mkuu hapo mwakani huku mmoja wa makada wa chama hicho akidaiwa kuendesha siasa zake kwa kutumia jina la mwenyekiti wa Chama hicho Taifa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kada huyo ambaye kwa sasa anatumikia adhabu baada ya kupewa onyo kutokana na kuendesha siasa zisizoendana na kanuni za viongozi na maadili za ccm na jumuiya zake toleo la 2022,ametajwa kutumia jina la kiongozi huyo kama kete katika harakati zake za kisasa.

"Hili jambo viongozi wa chama wilaya na mkoa wanalijua na wanahitajika kuchukua hatua,haiwezekani mtu atumie jina la kiongozi wa kitaifa kujinadi hii ni ukosefu wa maadili na ni kinyume kabisa na misingi ya chama chetu",anasema mmoja wa makada wa CCM aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Mbali na hilo, kada huyo pia anadiwa kutumia kete ya udini akiwaaminisha watu kuwa kwa vile mwenyekiti wa chama Taifa ni mwislam basi ni rahisi yeye kupenya kwenye kura za maoni na kupeperusha bendera ya chama cha mapunduzi kwenye uchaguzi mkuu.

"Wewe fuatilia kwa karibu,amekuwa akiwaonyesha watu simu ya rais akidai huwa anwasiliana nae mara kwa mara,hii siyo sawa hii ni kutumia vibaya jina la rais wetu na pia ni kukipaka matope chama kuona kwamba viongozi wanawatu wao kumbe sivyo"

KANUNI ZA UONGOZI NA MAADILI ZA CCM NA JUMUIYA ZAKE ZINASEMAJE?

Kanuni za uongozi na maadili za ccm na Jumiya zake toleo la 2022 zimeainisha mambo yasiyoruhusiwa ambayo mwanachama wa ccm anayetarajiwa kugombea nafasi ya uongozi eneo husika haruhusiwi kuyafanya.

Moja ya mambo hayo ni pamoja na utoaji wa michango,misaada au zawadi za vifaa au nyenzo kwa mtu au shughuli yeyote mpaka iwe tu kwa ridhaa ya kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya ngazi inayohusika kwa masharti kwamba kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa inapata taarifa.

Kwa kuzingatia kanuni hiyo sehemu ya 6 {2} {C} kada huyo wa ccm amekuwa akijihusha na utoaji wa michango katika maeneo mbali mbali misaada,zawadi.

Kwa faida ya wasomaji wa ukurasa huu tunaiweka kanuni ya 6{2}{c} kama inavyojieleza

{2} Kwa hvyo mwanachama haruhusiwi kufanya yafuatayo

{c} Kutoa michango,misaada au zawadi za ivfaa au nyenzo kwa mtu au shughuli yeyote mpaka iwe tu kwa ridhaa kamati ya siasa ya Halmashauri kuu ya ngazi inayohusika kwa masahrti kwamba kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa inapata taarifa.

Kutoka michnago,misaada,zawadi nk.katika eneo ambako mwanachama huyo anakusudia kugombea nafasi yeyote ya uongozi na endapo katika mazingira maalumu ruhusa imetolewa kama ilivyofafanuliwa katika vifungu 6{2}{a} na 6{2]{b}basi mchango huo hautatangazwa.

Tarfiak utoka ndani ya ccm Moshi mjini na ccm mkoa wa kilimanjaro zinapasha kuwa tayari malalamiko juu ya kada huyo kwenda kinyume na kanuni hizo yameshawasilishwa makao makuu ya chama Taifa na nakala ya malalamiko hayo kuepelekwa wilayani na mkoani kwa ajli ya hatua zaidi.

Inaelezwa kuwa kama tuhuma hizo zitadhibitika,kada huyo atakabiliwa na adhabu kali ambayo ni kupewa kalipio adhabu ambayo ni ya juu kabla ya kufukuzwa uanachama.

"wana moshi tunahitaji siasa safi, watu wanadi sera zao kistaarabu lakini si kwa kutumia mbinu ambazo zinakiuka kanuni za maadili"anasema kama wa ccm moshi mjini.

Tukiachie chama sasa kitafakari hayo yanayofanywa na kada huyo je hayakiuki kanuni hizo ama la
 
Back
Top Bottom