A
Anonymous
Guest
Wananchi wa Shabaha wanateseka sana na barabara iwe kipindi cha mvua au kiangazi kipande cha barabara mwisho wa Kituo cha Bajaji Shabaha.
Kuna barabara inaitwa Manguzoni kuelekea TPC Mita 700, imeharibika sana sana, ni barabara kubwa inayounganisha barabara ya lami kuelekea Moshi Mjini.
Gari, bajaji, pikipiki, baiskeli na Watembea kwa miguu, huwa mvua ikinyesha barabara haipitiki imechimbika sana.
Ujumbe uwafikie wahusika waitengeneze barabara hii, maana ndio barabara kubwa inayounganisha barabara mbili za kwenda Moshi Mjini.