A Anonymous Guest May 21, 2024 #1 Nina wiki moja nimekuja Moshi, nimetembela baadhi ya sehemu za Wilaya ya Moshi Vijijini, Shabaha, Kata ya Mabogoni. Wananchi wa Shabaha wanateseka sana na barabara iwe kipindi cha mvua au kiangazi kipande cha barabara mwisho wa Kituo cha Bajaji Shabaha. Kuna barabara inaitwa Manguzoni kuelekea TPC Mita 700, imeharibika sana sana, ni barabara kubwa inayounganisha barabara ya lami kuelekea Moshi Mjini. Gari, bajaji, pikipiki, baiskeli na Watembea kwa miguu, huwa mvua ikinyesha barabara haipitiki imechimbika sana. Ujumbe uwafikie wahusika waitengeneze barabara hii, maana ndio barabara kubwa inayounganisha barabara mbili za kwenda Moshi Mjini.
Nina wiki moja nimekuja Moshi, nimetembela baadhi ya sehemu za Wilaya ya Moshi Vijijini, Shabaha, Kata ya Mabogoni. Wananchi wa Shabaha wanateseka sana na barabara iwe kipindi cha mvua au kiangazi kipande cha barabara mwisho wa Kituo cha Bajaji Shabaha. Kuna barabara inaitwa Manguzoni kuelekea TPC Mita 700, imeharibika sana sana, ni barabara kubwa inayounganisha barabara ya lami kuelekea Moshi Mjini. Gari, bajaji, pikipiki, baiskeli na Watembea kwa miguu, huwa mvua ikinyesha barabara haipitiki imechimbika sana. Ujumbe uwafikie wahusika waitengeneze barabara hii, maana ndio barabara kubwa inayounganisha barabara mbili za kwenda Moshi Mjini.
Smith Rowe JF-Expert Member Joined Sep 18, 2018 Posts 4,570 Reaction score 9,778 May 21, 2024 #2 Mabogini sio Mabogoni. Toka nizaliwe sijawahi pita barabara mbovu kama hii unaweza ukahisi unaelekea kuzimu.
Mabogini sio Mabogoni. Toka nizaliwe sijawahi pita barabara mbovu kama hii unaweza ukahisi unaelekea kuzimu.