OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Mandhari saaafi ya ukumbi
Tukio hili lipo mubashara Azam TV
Tayari mgeni rasmi Mh.Spika Job Ndugai ameingia na shughuli zimeanza rasmi. Tukio limefana hakuna mfano
Updates
Mo Dewji agusia usajili Simba Sc
Mohamed Dewji ametoa neno kuhusu mipango ya usajili ndani ya timu hiyo na kusisitiza kuwa bajeti ya usajili msimu huu itakuwa mara mbili ya ile ya msimu uliopita.
Mo Dewji amezungumza hayo muda mfupi kabla ya kutolewa kwa Tuzo za Mo (MO Simba Awards 2019) zinazofanyika leo kwenye Hotel ya Hyatt Jijini Dar es Salaam.
Amesema mipango waliyonayo kwanza ni kuhakikisha wachezaji wote wazuri wanaendelea kubaki ndani ya Simba na kisha kusajili wachezaji wengine wapya wenye uwezo huku akisisitiza kuwa hadi sasa bado hawajaanza mchakato wowote wa usajili likiwemo suala la Nahodha wa Yanga Ibrahim Ajibu ambaye anahusishwa kujiunga na timu hiyo.
Updates
1. Tuzo ya golikipa bora amechukua Aishi Manula
2. Tuzo ya beki bora amechukua Erasto Nyoni