Most confusing and plot twisting series ever

Most confusing and plot twisting series ever

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Posts
35,812
Reaction score
107,628
Hello there....đź‘‹đź‘‹
Hua napenda nikikutana na series au muvi nzuri nishee nanyi “wakulungwa” wapenda motion pictures maana sharing is caring, I scare because I care.
Hua napenda series na muvi ambazo ukitazama unakua unakuna kichwa kuielewa, muvi zenye plot twisting na brain storming. Baadhi ya muvi nilizozipenda wa kutumia akili kubwa kwenye matukio yake ni dark knight,inception, Doctor strange, Tenet, interstaller,momento, Vantage point. Ukiangalia kwenye hio orodha muvi nyingi zime-directed na Christopher Nolan huyu mwamba anajitahidi sana kutengeneza muvi zenye kuchanganya.

Inception ukiangalia inabidi ukae na notebook kabisa nadhani hii ndio muvi yenye kuchanganya zaidi. Tenet inachanganya sana lakini kwa mtu aliyeitazama Doctor strange atagundua muvi hizi zinataka kufanana maana zote zinahusu time travelling wanapambana na matukio yaliyokwishatokea.

1620491812279.png

Tenet ni nzuri ila writing yake ni hovyo, sasa bwana nilikutana nah aka kaseries Netflix kanaitwa Dark niseme tu hakuna muvi au series yenye kuchanganya kama hii yaani ukiangalia inabidi uwe makini sana. Series iko serious muda hakuna kucheka wala kutabasamu unabaki kwenye suspence muda wote.
Kuwafahamu character tu inachanganya maana character moja imechezwa na watu watatu ambapo wamegwanywa sehemu tatu ambazo ni Teen,adult na elder imetengenezwa na wajerumani…


Jonas Kahnwald (huyu ndio sterling)
Teen: Mwanafunzi wa sekondari ambae baba yake alijinyonga
Adult: mwanaume anayetoka future anakuja kumtembelea Jonas akiwa teen(time traveler)
Elder: Kiongozi wa kikundi cha Sic mundus ambae anajiita adam

Hannah Kahnwald:
Teen: mtoto wa Sebastian kruger ambae ana wivu na usiri sana
Adult: mama yake na Jonas ambae anafanya kazi ya massage

Ines Kahnwald
Teen: mama mlishi wa Michael ambae ni Nesi
Elder: bibi yake na Jonas

Martha Nielsen:
Teen: mtoto wa Katharina na Ulrich Nielsen anayesoma sekondari ni mpenzi wa Bartoz lakini pia wanapendana na Jonas

Magnus Nielsen
Teen: mtoto mkubwa wa Katharina na Ulrich Nielsen anayesoma sekondari ni mpenzi wa franziska

Mikkel Nielsen:
Teen: mtoto mdogo wa Katharina na Ulrich Nielsen aliyepotea mwaka 2019 akatokezea 1986
Adult: Mume wa Hannah na baba wa Jonas ambae alijinyonga

Ulrich Nielsen
Teen: mwanafunzi wa sekondari ambae mdogowake alipotea
Adult: Mume wa Katharina na baba wa magnus,Martha na mikkel anafanya kazi ya upolisi

Katharina Nielsen
Teen: mwanafunzi wa sekondari na mpenzi wa Ulrich
Adult: mwalimu mkuu wa sekondari ambae ni mke wa Ulrich na mama wa magnus,mikel na Martha
Niishie hapa maana character bado ni wengi halafu wanauhusika tofauti tofauti ila nadhani mpaka hapo nimeweka wale wa muhimu zaidi mwisho nitaweka family tree.

Nchini german katika mji mdogo uitwao winden mji huo ulikua umezungukwa ni misitu, ili kufika shule ilitakiwa upite kwenye msitu huo pia kwenye msitu huo kulikua na kituo cha kufua umeme( power plant) ambacho kilikua hakifanyi kazi kwa miaka ya sasa lakini pia pembeni ya kinu hicho kulikua na pango kubwa kiasi vjana watundu walipenda kwenda kupiga stori na kuvuta mjani nje ya hilo pango.

June 2019 Michael Kahnwald anajinyonga akaacha barua ikiwa imeandikwa isifunguliwe mpaka ikifika Novermber 4 2019, baada ya kifo cha Michael mwanae Jonas anapata ugonjwa wa akili. Baada ya kifo cha michael mkewe Hannah kahnwald anaanza mahusiano na afisa polisi aitwae Ulrich Nielsen. Baada ya miezi miwili toka kifo cha baba yake Jonas anatoka kwenye hospital ya wagonjwa wa akili anaenda shuleni na kuungana na marafiki yake ambae ni Bartsoz, Jonas alipoenda shule alikuta kuna jamaa anaitwa Erik aliyekua anawauzia bangi shuleni kapotea kwa siku mbili.

Bartsoz akawaambia Magnus,Jonas franziska na Martha kwamba anajua Erik alipokua anaficha bangi na hela huko kwenye msitu karibia na pango hivyo waende wazichukue wakakubali wakaenda mdogo wao Mikkel akaomba naye awafuate huko msituni wakamkubalia…ikumbukwe Bartsoz mpenzi wake ni Martha ila Martha anampenda Jonas pia.
Walipofika huko msituni wakasikia sauti ya ajabu wakaanza kukimbia katika kukimbia Mikkel akapotea, Ulrich ambae ni polisiakachanganyikiwa anamtafuta mwanae kila sehemu ikumbukwe pia Ulrich aliwahi kumpoteza mdogo wake mwaka 1986 aitwae Mads Nielsen, Katika kumtafuta mwanae kule kwenye pango akagundua kwamba kuna mlango upo ndani ya pango hilo ambao unaonyesha ukipita huo mlango unatokezea kwenye kile kituo cha kufua umeme hivyo ikabidi aende kuomba kiongozi wa kituo ambae ni alexander tiedman ambae ni baba yake na Bartsoz amruhusu aingie ndani ya kituo ila alikataliwa.

Siku mbili baada ya kupotea mikkel a
Unapatikana mwili wa kijana/teen ameungua usoni na masikio yake yameharibiwa. Mkuu wa polisi ambae ni Charlotte dopler anaambiwa kwamba mwili wa mtoto huyo unaonyesha amekufa masaa 16 yaliyopita ila kavaa nguo za kipindi cha miaka ya 80.

Mikkel anashtuka alipokua amenguka kule porini baada ya kukimbizwa anaenda shuleni anakosoma ambapo mama yake ndio mkuu wa shule anaenda kumuulizia lakini katika kutafuta akagundua kwamba tarehe ya siku hiyo ni November 5 mwaka 1986 wiki mbili baada ya kupotea kwa Mads Nielsen (ambae ni baba yake mdogo mikkel), sasa dogo kachanganyikiwa polisi mmoja ambae ni eogon tiedman alivyomuona mikkel kaumia halafu maelezo yake hayaeleweki kwao ni wapi akahisi atakua kaumizwa na kijana mtukutu wa eneo hilo ambae ni Ulrich mikkelson hivyo aliitwa na kuhojiwa. Polisi alimpeleka mikkel hospital akapokelewa na Ines kahnwald, mikkel kwakua alikua ni mtoto anaependa kusoma soma aligundua kwamba karudi wakati uliopita/past na hawezi kurudi tena alipotoka mwaka 2019 hivyo Yule nesi Ines akajitolea kumlea kama mwanae.

Mwaka huo huo kuna mchungaji anamtembelea mikkel hospital anajitambulisha kua anaitwa Noah.
Tukirudi 2019 kuna mtoto mwingine anaitwa Yasin anapotea, katika hotel moja The stranger (time traveller) anamwambia muhudumu wa hotel ambae ni Regina Tiedman ambae ni mama wa Bartsoz kwamba ampetie mzigo Fulani Jonas. Jonas akiwa kwenye kaburi la baba yake akafuatwa na The stranger akamwambia kwamba baba yake Jonas aliwahi kumuokoa kipindi kimoja.

Bartsoz alikutana na jamaa ambae yeye ndio alikua anasambaza madawa na bangi wamuuzie jamaa huyo alijitambulisha anaitwa Noah Yule aliyeenda kumuona hospital mikkel mwaka 1986 kavaa kama mchungaji.Jonas aliupokea mzigo ulikua na ramani taa na vifaa kadhaa, Jonas akafungua ile barua aliyoacha baba yake kabla ya kujiua inasema kwamba November 4 mwaka 2019 alisafiri mpakamwaka 1986 ambapo huko alikaa na kukua akilelewa na ines akamuoa Hannah.

1620491996863.png

Hivyo basi Yule mtoto Mikkel Nielsen mtoto wa Ulrich Nielsen aliyepotea mwaka 2019 akatokezea mwaka 1986 alikaa hukohuko akabadirisha jina akaitwa Michael Kahnwald akamuoa Hannah kisha wakazaa mtoto aitwae Jonas Kahnwald. Ikumbukwe wakati mikkel anapotea akiwa mdogo walikua pamoja na Jonas kule msituni. Kwahiyo Ulrich ni babu yake na Martha ambae Jonas walikua wanapendana kwa siri ni shangazi yake.

Hivyo mikkel alisoma shule moja na baba yake na mama yake pia walichnagia demu mmoja na baba yake ambae ni Hannah, Hannah alikua na mahusiano kwa siri na Ulrich walipokua vijana/teens hata baada ya mikkel kujinyonga 2019 waliendeleza
Jonas alienda kwenye lile pango akatokezea mwaka 1986 akiwa njiani alipewa lift na mzee mmoja ambae ni baba wa binti aitwae Hannah..hnnah alikua ndani ya gari pia hivyo akakaa na mwanae bila kujua Jonas akaenda shuleni akamuona Mikkel shuleni akataka aende amchukue amrudishe mwaka 2019, Yule the stranger akamziwia akamwambia kwamba kama akimrudisha mwaka 2019 basi mikkel hawezi kumuoa Hannah, kama hata muoa Hannah basi mikkel hatazaliwa.

Yule the stranger ni Jonas kutoka Future kwahiyo pale walikuwepo Jonas wawili kijana wa 2019 na mtu mzima wa 2040s. Yule mtu anayejitambulisha kama mchungaji noah ambae alikua kamchukua bartsoz amuuzie madawa, kumbe alikua ni mtoto wa bartsoz ambae nae alikua anashiriki kupoteza watoto kwa na kuwaua kwa mitambo walikua wanawatoa mwaka 1986 wanawaleta 2019 wangine wanawatoa 2019 wanawapeleka 1953.

Iligundulika kwamba kila baada ya miaka 33 lile pango kule msituni hua linakua na Wormhole ambayo huwezesha watu kusafiri katika muda (time travelling)
Anayependa series za kuchanganya aingalie hiii hope utainjoi sana hayo niliyoelezea nimeacha matukio meeengi tu muhimu tena nimeeleza matukio baadhi ya episode kama 6 kutoka season 1 zipo season 3 kila moja ina ep 3. This is one of the best series I ever come across.
 
Katika mambo ambayo siwezi kufatilia wala kuangalia ni "Movies" yaani kitu chochote ambacho huwa kinahusu maigizo siwezi labda sababu napenda sana uhalisia kuliko sanaa.

Huwa niashi na kauli ya Mwanachuoni mkubwa sana kutokea nchini Albania aliyefariki mwaka 1999, anasema :

"Filamu au maigizo ni jambo baya na lenye kuchukiza sababu hupunguza katika ukweli au huongeza katika ukweli bali hupotosha kabisa" (Au kama alivyo sema).

Endeleeni kula maisha waungwana. Sisi tuko huku.

Shikrani.
 
Kiukweli mimi napenda movie/series ambazo sitoweza ku-predict matukio yake ya mbele.

Nikitazama movie/series toka episode ya kwanza huwa nakuwa na-predict matukio yanayofata sasa mawazo yangu yakiweza kufanana na director hakika hiyo series/movie lazima nitaiona mbovu.

Napenda sana director aweze ku-twist story zaidi ya mimi navyofikiria.

Hiyo ndio changamoto inayonisumbua imesababisha niwe na Series/Movie chache nazozikubali baada ya kuzitazama na zingine kuziona mbovu kabisa.

Mfano wa series bora kwa upande wangu: Peaky blinders, GOT, The Witcher, The Originals, The Shadow and bones na zingine kama hizi.
 
Ndiyo mambo ya grandfather paradox nini? Kwa ulivyoielezea nimeipenda sana.
 
Niwe mkweli tuu hii series ya Dark niliiangalia lakn sijaielewa kabisa, Ila pia nimekuja kugundua series nyingi za time travelling zinahitaji umakini na uelewa mkubwa hasa wanapohusisha mhusika mmoja katika matukio na muda tofauti
 
sijui kwanini recent nimejikuta siwezi kuangalia series kama tu haihusu madawa ya kulevya au any gang related activity..

-power

-power book 2

-narcos

-narcos mexico

-gang related

-ozak

-zero zero zero

-gangs of london

-woman of steel

-queen of the south

-el chapo

-cocaine coast

-the club

-undercover

-how to fix a drug scandal

and the likes
 
Asante! Wacha niitafute kwa jinsi ulivyoelezea inaonekana iko vizuri
 
Ong
sijui kwanini recent nimejikuta siwezi kuangalia series kama tu haihusu madawa ya kulevya au any gang related activity..

-power

-power book 2

-narcos

-narcos mexico

-gang related

-ozak

-zero zero zero

-gangs of london

-woman of steel

-queen of the south

-el chapo

-cocaine coast

-the club

-undercover

-how to fix a drug scandal

and the likes
Ongeza na Breaking bad Mkuu
 
Kabisa mate, Series au muvi za time traveling hua ni mgumu sana kuzielewa.
  • Tenet
  • Doctor strange
  • Avanger endgame
  • Time traveler's wife
  • Looper
  • Nk nk
Tenet Ni mbaya sana sjui watu wanaisifia nini ila nyengine zinaeleweka
 
Get out ya 2017 nai recommend hii nzuri sana ina plot twist

Hii movie

inaweza kuonekana kama filamu nyingine ya kutisha, lakini inaishia kuwa na mambo mengi [emoji3].

Daniel Kaluuya ana act kama kijana Mweusi anayeenda kukutana na wazazi wa rafiki yake wa kike mweupe ndani ya katikati mwa kitongoji tajiri chenye wakazi wengi wenye rangi nyeupe.

And then plot inakuwa twisted vile unavyofikiria inaenda kuwa ni tofauti
 
Hii series kwa maandishi sidhan kma kuna MTU anaweza ielewa.hii ni series imedeal na concept za muda, paradox,loop.nilivyomaliza season 2 theme iliyotumika kwenye tenet "what happened happened" nkajua everyone one is bound to make the same mistake, season 2 mwishon ndio imekuja kubadilika ambpo walitambulisha alternate universe na loop hole ambay Adam alikuwa haijui ila Eva ndio alikuwa anaitumia kwa faida zake kma kumuokoa Jonas na kufnya kaz na Claudia

Season 3 ndio ilianza kwa kunichanganya ila nlikuja kurud kwa theme ya series kwamb what happened happened maana kwney winden ya Eva mambo yalikuwa yanajirudia vilevile sema baadh ya vitu vlikuwa tofauti mfano Jonas hakuwa hayupo maana mikkel hakisafiri kurudi nyuma.

Kama ningesema nitoe pongezi kwa hii series ningezipeleka kwa Claudia maana yeye ndio alieweza kujua jinsi ya kuvunja knot na cyle.

Nliyofika scene za mwisho nlijua kutakuwa na season 4 maana mwishon kule Hannah kulikuwa kuna kitu tunaita glitch in time maana tuliona Hanna alikuwa na deja vu alivyoona koti ambalo Jonas alikuwa akivaa, pia alipoulizwa jina la mtoto ataitwa nan akasema Jonas.

Sema ndio wameishia hapo,nliienjoy sana kuangalia hii series

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom