Most corrupt Nations??

Most corrupt Nations??

Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Posts
3,154
Reaction score
71
Pamoja na EPA na nini lakini hatuko kabisaa kwenye hii list Transparance intenational...
1. Haiti
2. Myanmar
3. Iraq
4. Guinea (Conakry)
5. Sudan
6. Democratic Republic Congo/Kinshasa
7. Chad
8. Bangladesh
9. Uzbekistan
10. Equatorial Guinea
11. Cote d'Ivoire
12. Cambodia
13. Belarus
14. Turkmenistan
15. Tajikistan
16. Sierra Leone
17. Pakistan
18. Nigeria
19. Kyrgyzstan
20. Kenya
21. Republic of Congo Brazzaville
22. Angola
23. Venezuela
24. Niger
25. Ecuador
26. Cameroon
Pengine hatutakiwi kulia sana tumpongeze rais aendelee kujitahidi asiwepo kwenye hii list...
 
wakati fulani nigeria ndio ilikuwa inaongoza duniani,,,,
nahisi watafanya sherehe kururahia kushuka chati....
 
lois farakhan aliwahi sema u.s.a ndio most corrupt nation in the world..
wapo watu wanafikiri inapaswa kuwemo kwenye list..
 
Tumain ndugu yangu katika hizo nchi ni ipi wanayopokea sana misaada toka kwa donors? ukiona donors wanajua wewe fisadi na still wanakupa misaada basi kuna kitu wanafaidi!

Jamaa walivyo na uchunguzi mzuri wangeisha sitisha misaada tangu miaka hiyo, lakini bado wanatoa!

hatuwezi kuwa humo hata kama ni wa kwanza
 
Ndugu wakati mwingine wanasema kweli nchi kama cameroun ni kweli kabisa nilikuwa huko huwezi toka uwanja wa ndege kama hujaachi kitu kidogo ($5) utazungushwa mpaka kieleweke.
 
Ndugu wakati mwingine wanasema kweli nchi kama cameroun ni kweli kabisa nilikuwa huko huwezi toka uwanja wa ndege kama hujaachi kitu kidogo ($5) utazungushwa mpaka kieleweke.

siyo tip? LoL!!, kumbe tuna afadhali, tukiondoa ccm tu na kuleta viongozi bora, nchi yetu itakuwa paradiso ndogo
 
mtego uliomnasa tumaini na wengine wanaoamini tafiti kama hizo ni uleule uliomnasa makapa na serikali yake. yaani takwimu. hayo ni matokeo ya takwimu na takwimu ni taarifa rasmi, hazijumiishoi taarifa zisizo rasmi. kwa nchi kama yetu ambapo kumbukumbu hufunikwa au haziwekwi sawa, au rushwa kwene maeneo remote hazijumuishwi, vinginevyo labda tungekuwa wa kwanza!

chukulia mfano kiongozi akianzisha kampuni (mfano kingunge ambaye wote tunamjua kuwa hana background ya biashara yoyote tangu ujana wake) basi husinda kila tenda nono na huku tukiambiwa alishindanishwa. kwa hali hiyo hakutawekwa takwimu hapo ya uwezekno wa rushwa.

mathalani mmbo ya 10% kwa kuwa yanafuata documentation nayo pia huwezi kukuta takwimu yake yakihusishwa na rushwa, lakini ni rushwa tena mbaya sana.

tuwe waangalifu na takwimu, ni mitego!
 
Back
Top Bottom