Mothers' Special Thread

Raymanu KE

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2022
Posts
8,611
Reaction score
16,118
Hamjamboni wanajamvi? Natumai mpo salama kbsa.

Huu uzi Ni maalum kwa ajili ya mama zetu.Tuchukue fursa hii kuwapongeza mama zetu kwa Yale mengi mazuri waliotufanyia mpaka tumefikia Hapa tulipo.

Wapo wenzetu ambao kwa Bahati mbaya waliondokewa na mama zao wapendwa na Basi tunawaombea kwa Mungu aendelee kuzilaza roho zao mahali pema peponi🙏

Naamini kila mmoja anaelewa Yale magumu na changamoto walizopitiq mama zetu kipindi wanatulea tukiwa wadogo.Akina mama wamejaaliwa sifa ya uvumilivu maana huwaga wanapitia mengi Sana.

Binafsi sijawahi kuona mwanamke mzuri kuwahi kuishi Hapa Duniani kumliko mama yangu.Naeza sema yeye Ni Mungu wangu wa pili baada ya Mwenyezi Mungu. Mama yangu ndiye mwanamke ninayempenda na kumheshimu Zaidi maishani mwangu.Indeed she's my role model na huwa namuomba Mungu kila siku ampe baraka ya maisha marefu Hapa Duniani yenye furaha tele na amani.

Kiukweli siwezi kuyaelezea mazuri yote aliyonitendea mama yangu pamoja na ndugu zangu watatu hata nikapewa fursa ya siku nzima.Ni mengi Sana kwa kweli. Mama yangu Ni mwanamke wa shoka.Ni mpambanaji kiutaftaji, amejitoa Sana kwa ajili yetu sisi wanae.Toka tunazaliwa mpaka tumekua wakubwa mama amekuwa katika mstari wa mbele kupigania haki zetu.

Zipo changamoto nyingi Sana ambazo mama yetu alikumbana nazo kipindi anatulea sisi.Mateso na manyanyaso( mengine kutoka kwa baba yetu) ambayo siwezi kuyaeleza hapa jukwaani ila mama yetu alikuwa jasiri Sana katika kupambana na hizo changamoto mpaka akashinda.

Basi wanazengo,tuchukue fursa hii kuwapongeza mama zetu kwa Yale mengi waliotufanyia na kuwaombea baraka tele kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Mungu mbariki Mama yangu.
🙏🙏
 
Mungu ambariki mama yangu kipenzi nampenda sana[emoji7]

Mungu awarehemu wamama wote waliotangulia mbele ya haki[emoji1545]

Mungu awape shifaa wamama wote,wanaosumbuliwa na maradhi,
 
Mungu ambariki mama yangu kipenzi nampenda sana[emoji7]

Mungu awarehemu wamama wote waliotangulia mbele ya haki[emoji1545]

Mungu awape shifaa wamama wote,wanaosumbuliwa na malazi.
Ahsay Sana kwa ujumbe wako mzuri mkuu🙏
 
Mungu ambariki mama yangu kipenzi nampenda sana[emoji7]

Mungu awarehemu wamama wote waliotangulia mbele ya haki[emoji1545]

Mungu awape shifaa wamama wote,wanaosumbuliwa na malazi.

Malazi au 'maradhi'?
 
"To describe my mother would be to write about a hurricane in its perfect power. Or the climbing, falling colors of a rainbow.” - Maya Angelou
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…