Tatizo sio wakwepa kodi tu,hicho kingi kinachopatikana kinatumika vipi ?
Kuna ubadhirifu mkubwa wa mapato ya serikali. Kama kuna upungufu wa mapato kulikuwa na haja gani ya mbwembwe za uhuru,haya ma vx,gx,bmw,benz,discover a.k.a SU na STK, yanatoka wapi kama tax evasion ndo tatizo peke yake.
Kupanga ni kuchagua ,tunahitaji kuwa na mipango thabiti ya ukusanyaji na matumizi sahihi ya mapato. Tukikusanya halafu zikaishia kwenye posho,posh cars,na other unneccessary expenditure hata mimi siwezi kuwa na moyo wa kutaja wakwepa kodi bali nitatafuta njia za kukwepa. Maisha ni magumu, kwa nini uzibe kwa wengine wakati kwako panavuja.