Motisha ya kazi ni pesa pekee?

kisokolokwinyo20

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2019
Posts
472
Reaction score
423
Habari ya asubuhi wakuu,

Ni hivi, hakuna mtu anaweza kufanya kazi bila ya kupatiwa motisha itakayoamsha Ari au Morali itakayoongeza kujituma na kuleta matokeo chanya katika Eneo lake La Kazi.

Lakini kuna zile 'theories' za motisha ambazo zimejaribu kuelezea vitu mbalimbali vinavyoweza kumpa nguvu zaidi ya kufanya kazi na kuridhika.

Ikumbukwe kuna motisha za aina mbili kuna Pesa (Financial) hapa ni kuwa na mshahara mzuri, kupandishwa cheo, bonasi na nyongeza za mishahara... Halafu kuna hio ambayo Sio ya Pesa ( Non Financial) hapa ni kama kupewa mafunzo, vitendea kazi, mazingira mazuri ya kazi, kupatiwa malazi, kutambulika pale unapofanya vizuri nakadhalika.

Naomba tuje kwenye uhalisia sasa, Jee, kwa mazingira yetu ya kila mmoja kazini kwake ni nini kinakupa motisha ya kazi??

Nawasilisha kwa michango ya Mawazo[emoji3578][emoji3578]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…