moto mkubwa UDOM{COED}

ndogwila

Member
Joined
Jan 10, 2011
Posts
21
Reaction score
3
Baada ya kile kinachodaiwa kushindwa kwa serikali legelege ya wanafunzi wa kitivo hicho, kusimamia msimamo wao wa wazirl mkuu mh.Pinda kuongea na wanafunzi wote,vilevile hasira kali zimeibuka miongoni mwa wanafunzi hao kwa kudai kudharauliwa na waziri mkuu.wanadai kuwa wamemsubiri kwa takribani wiki nzima na matokeo yake amewapita kama vile mtalii anavyoangalia wanyama mbugani.
 
Kwa hiyo kama pinda amewa\ ignore wamewasha moto gani?
 
Amehisi wanamuuliza haki zao na masuala ya Dowans!
si unajua serikalini sasa wanakimbiana?
Yeye anadhani kutatua kero na UDOM-utawala ndio amesawazisha mambo! la, wanafunzi ni zaidi ya utawala. wao ndio waathirika wakubwa.
 
aggggh,title ya thread na content ya thread tofauti
 
HII THREAD IMEANDIKWA NA MWANAFUNZI WA CHUO CHA KATA. Kumbuka huo mgomo ni wa WAHADHIRI na sio wa WANAFUNZI.
 
We mtumpole ndo ujui kitu ni bora unyamaze...! nenda college of education kule udom alafu ujue kama mgomo ni wa wanafunzi au lecturers...kwa hali ilivyo,hata lecturers wakitatua matatizo yao,bado mgomo uko pale pale kutokana na matatizo yaliopo kwa wanafunzi...
 
UDOM inabidi mjipange ili kuinua status ya hiko chuo.Inaelekea serikali imewekeza sana kuboresha majengo than academic issues hapo chuoni.
 
HII THREAD IMEANDIKWA NA MWANAFUNZI WA CHUO CHA KATA. Kumbuka huo mgomo ni wa WAHADHIRI na sio wa WANAFUNZI.
Mtupole, Una uhakika??.. be sure of what ur posting!....
 
wanataka kupumzika hao, ningewaona wa maana kama wangegomea na DVC taaluma naye aondoke kwa kuzorotesha taaluma ukianzia na prospectus ambayo ni chanzo cha mkanganyiko mkubwa wa degree program nyingi hapo chuoni, semester fupi, degree program bila TP, degree utititri zisizo na walimu wa kutosha.
 
Pinda ametatua mgogoro uliokuwepo kati ya menejiment na wahadhiri.Walioandamana mpaka ofisini kwake huku wakipigwa mabom ni wanafunzi wa COED.Amefika mpaka chuo na ameignore kuöngea na wanafunzi kitu ambacho kimewakasirisha zaidi.Uongozi wa wanafunzi usioungwa mkono hata kidogo kwa sasa ndio ulioteta na Pinda kinyume na matakwa ya wanachuo kwamba aongee na wanafunzi wote COED.Kila siku kuna vikao vya wanafunzi kuamua mustakhbali wao na tayari wameridhia kwa kauli moja tangu juzi kuitoa serikali madarakani na kuweka viongozi ambao wana imani nao.Mgogoro uliopo kwa sasa ni uongozi usiotakiwa kuendelea kushikilia ofisi huku wakitakiwa kukabidhi.Hakuna masomo yanayoendelea leo ingawa walim wamekuja kwakuwa bado kilichogomewa wiki nzima hakijatokea.Ambao wamepelekea hali hii ni viongozi ambao wameshindwa kusimamia maslahi ya uma uliowaweka madarakani na kuendeleza unafiki mbele ya menejimenti.Jamii isiamini kwamba Pinda amemaliza mgomo wa wanafunzi,aliofanikiwa kuumaliza ni ule wa wahadhiri.Madai ya msingi ya wanafunzi college of Education ni haya:Kurudishiwa fedha ya acomodation iliyozidi;Kudai fedha ya mahitaji maalum ya kitivo;Mikopo;Kukoma tabia iliyozoeleka ya kusoma kozi ya semista nzima kwa wiki moja au mbili.Hii ni kwa zile kozi ambazo hazina waalim eg.PHYSICS.Wanafunzi wanaona bora chuo kizifute kozi hizi kuliko kuendelea na mtindo huu mbovu na wapekee!;Miund6binu duni;Maji;Kuachia ngazi mnyanyasaji mwizi na jambazi katili Prof.Mlacha;Na mengineyo.Bila haya kutatuliwa wanafunzi wataendelea na mgomo mpaka kieleweke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…