Moto ulioteketeza wanafunzi ulianzishwa kimaksudi

Moto ulioteketeza wanafunzi ulianzishwa kimaksudi

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Moto uliozuka katika shule ya upili ya wasichana ya Moi jijini Nairobi jumamosi asubuhi ulianzishwa kimaksudi na haikuwa ajali. Akihutubia wanahabari hivi leo, waziri wa elimu Dr Fred Matiangi amesema kufikia sasa idadi ya wanafunzi waliofariki kwenye mkasa ahuo imefikia wanafunzi-9 baada ya mwanafunzi mwengine kufariki kutokana na majeraha ya moto. Hospitali ya Nairobi Women imethibitisha kwamba wanafunzi wawili kati ya kumi waliolazwa katika hospitili hiyo kufuatia mkasa huo, wangali katika hali mahututi. Kwa sasa uchunguzi wa DNA unafanywa kuwezesha wazazi kutambua watoto wao na kuandaa mazishi. Shule hiyo imefungwa kwa muda wa majuma mawili huku uchunguzi kuhusu mkasa huo ukiendelea.

CHANZO: Radio Taifa
 
Back
Top Bottom