08 April 2025
Dodoma, Tanzania
Katika hali isiyo ya kawaida mbunge aomba bunge lisitishwe ili lijadili barabara ya kutoka Dar es Salaam hadi Mtwara iliyokatika katika Daraja la Somanga Mtama
View: https://m.youtube.com/watch?v=_BOrxz9JsPk
Ziara ya kikazi ya CHADEMA mikoa ya Kusini wamekuwa wakiwauliza watanzania wa mikoa ya Lindi na Mtwara imeikosea nini serikali ya CCM haidi ikawapuuza katika barabara, korosho, mbaazi na ufuta bila kusahau gesi.
Kupitia ajenda ya kudai Mabadiliko - No Reforms No Election 2025, CHADEMA imesema wananchi hao ndiyo wanaweza kupata wawakilishi wao waliowachagua kuanzia ngazi ya uongozi ya, vijiji, udiwani na ubunge ili kuweza kuibana CCM...
TIMU MAHIRI INAYOJUMUISHA TUNDU LISSU, JOHN HECHE, GODBLESS LEMA NA VIONGOZI WA KIKANDA NA MIKOA YALETA BALAA KWA CCM
Sasa hivi tegemea vituko na hao wabunge kujifanya wana uchungu sana na wananchi wao ili warudi tena, utawaona wanalia kuonesha wanavyoumiq, mara kushika shilingi na vibweka kedekede ili kuwahadaa wapiga kura
Hata wale waliokuwa mabubu sasa watapokea uponyaji wataongea
Wamekurupuka bungeni Dodoma baada ya kuona ukweli kuwa wabunge wamekuwa watetezi wa Mama na serikali ya CCM miaka yote badala ya kuwa watetezi wa wananchi
Katika mada aliyotoa tarehe
31 March 2023 yaani miaka miwili iliyopita (leo 2025) kwa hadhira ikiyofika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), iliyokuwa imeandaa mjadala wa miaka 30 ya demokrasia ya Tanzania katika Ukumbi wa Kisenga LAPF Conference Center, Jijini Dar es Salaam ....
Ujumbe mzito wenye ushahidi unaonesha kuwa Watawala wanasisitiza Amani kuliko Haki.. anafafanua askofu Bagonza,...
N.B mwaka 2025
Hivi kweli waTanzania tutegemee HAKI leo 2025 tukielekea uchaguzi wa 2025 huku tuna ushahidi usio na shaka wa Uchafuzi wa chaguzi za 2020, 2024 TAMISEMI ila tunapenda kujisaulisha kuwa kuna mabadiliko bila shindikizo la NO REFORMS NO ELECTION 2025 kufanyiwa kazi?