Moto wa Muswada wa Katiba wahamia visiwani zanzibar

Moto wa Muswada wa Katiba wahamia visiwani zanzibar

MWALLA

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2006
Posts
16,952
Reaction score
10,500
MOTO WA MSWADA WA KATIBA WAHAMIA VISIWANI ZANZIBAR

Chama cha Wananchi (CUF) kimemtaka Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, kujiuzulu wadhifa huo kwa kushindwa kusimamia maslahi ya Zanzibar. Kauli hiyo ilitolewa mjini Zanzibar jana na Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF, Ismail Chusa Razu, wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kibanda Maiti.

Alisema Balozi Seif amegeuka dalali wa kuiuza Zanzibar baada ya kukiri kuwa Zanzibar ilishirikishwa katika Mswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Muungano katika kipengele kinachohusu Zanzibar, jambo ambalo sio kweli. Aliongeza kuwa, Balozi Seif akiwa kiongozi alistahili kuzungumza na Waziri wa Katiba na Sheria pamoja na Mwanasheria Mkuu ndipo apate cha kuzungumza.

"Namtaka Balozi Seif ajiuzulu nafasi yake kwa kushindwa kusimamia maslahi ya Zanzibar, ikiwa ana uchungu wa Zanzibar hakustahili kusema hivyo," alisema na kuongeza kuwa kuanzia sasa watakuwa wakimuita Balozi Mkazi wa Tanganyika na Zanzibar. Kwa upande wa kada mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombale Mwiru,kusema anashangaa wazee wenzake kuleta rasimu ya Serikali tatu wakati Serikali mbili zilizopo kila moja ina mipaka yake na Zanzibar na bara zilikufa mwaka 1964 wakati nchi mbili zilipoungana,Chusa alisema Zanzibar bado ipo hai na itaendelea kuwa hai hadi kiama.

Alisema iliyokufa ni Tanganyika hivyo kama lengo ni kuizika Zanzibar bado hawajafanikiwa kwani Wazanzibari wapo macho.

"Zanzibar ipo hai na itaendelea kuwa hai hadi kiama, nchi hii haijazikwa," alisisitiza. Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad, alimtaka Rais Jakaya Kikwete, asisaini mswada huo, kwani ana nia nzuri, lakini wenzake wanataka kumpeleka kubaya.

"Rais Kikwete ana nia nzuri lakini wenzako wanakupotosha, usisaini mswada huu tunajua una nia nzuri,"alisema Maalim Seif na kuongeza kuwa iwapo atakubali kusaini mswada huo atazuia wajumbe wa chama hicho wasishiriki Bunge la Katiba. Alishauri mswada huo urejeshwe Zanzibar ili kupata Katiba Bora. Kuhusu Balozi Seif, Maalim Seif alisema anamuonea huruma makamu mwenzake huyo kwa sababu hakujua ni mswada upi aliuona.

Alisema Mei 6, mwaka huu aliitwa Dodoma na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kuambiwa kuwa wanataka kufanya marekebisho kwenye vipengele sita ambapo walifanya marekebisho, lakini waliporudi Tanzania Bara walifanya marekebisho kwenye vipengele nane. Alisema makamu wake hakujua hilo na anashangaa ni kwa nini wana-CCM wenzake wamemtosa. Alisema bila shaka walikuwa wamepanga jambo hilo.

Alisema Waziri wa Sheria na Katiba Zanzibar, Mwanasheria Mkuu, Rais wa Zanzibar na yeye mwenyewe hawakubaliani na hilo.
 
Ngoma ikilia sana mwisho huzaa ngoma zingine nyingi, hii nayo ngoma hata kama ni kadogo
 
Janja Janja hizi za CCM-Bara Zinaweza zisiwasaidie, Watu wamebadirika, mazingira ya siasa yamebadilika sasa hizi Janja-Janja na Ngiriba walizozizoea CCM zinaweza zikawapeleka pabaya...Sasa si ni aibu hata wanauziana mbuzi kwenye gunia na washirika wao wa Zanzibar. Basi ngoja tuone mziki huu utaishia wapi, Kuna mawili CCM wafanikiwe na nchi ibasuke ama CCM wakubali kushindwa tuendelee kuwa wamoja na Amani. Let us wait and see time will tell.....
 
Naichukia sana CCM kwa kitendo chake cha kuteka nyara nchi hii na kutaka kuteka haki za watanzania wote maccm exclusive, Siungi mkono tabia hizi za wabunge wa ccm kwa jinsi wanavyotunyanyasa hasa sisi watanganyika. CCM ife tu ili watu tuishi.
 
ngoma inogile,ngoma imekolea ngoma ya katiba ahahaha CCM mmeliwa
 
kila linalofanywa na viongozi wa ccm linkuwa ni chukizo kwa watu, ccm ni sikio la kufa, na kama wanataka kujizika kabla ya 2015 wafanyee maandamano ya kuunga mkono rasimu ya katiba lakini kwa kuwa ni sikio la kufa wanaweza kufanya hivyo
 
Hua sielewi ccm hasa hua inasimamia maslahi ya nani? Wananchi wenyewe wamesema wanataka serikli 3, wao hawataki, sasa wanamuongoza nani? Ningependa Nape uje uchangie na huu uzi cause we kila kitu hua unabisha tu.
 
CCM wabaya jamani, wanamsaliti hadi mwana CCM mwenzao!
Prof. Lipumba.
Sep 21, Jangwani.
 
Mpaka maalim seif ameshitukia, ccm wana mpango wa kumvurugia kikwete ili katiba mpya isipatikane!
 
Moto moto unguza ccm hao.mpaka kieleweke.
 
Hiyo ndiyo Ccm,ni waongo,matapeli,majizi,wanajua Katiba mpya inakuja kuwanyang'anya ulaji.kazi kupeana vyeo tu,sasa Kama mwanaccm mwenzao wamemdanganya,unategemea mwananchi wa kawaida wakueleze ukweli kwenye mikutano Yao.subiri Katiba ya ukweli ije kitaeleweka tu,hivi wakuu wa wilaya wanakazi gani?wamegeuka kuwa wanasiasa,hata ukiwauliza kazi zao,wenyewe wanakiri hawajui,yaani wapo wapo tu,wanasubiri kupokea mwenge kwenye wilaya zao,mafisadi
 
Back
Top Bottom