Mourinho for England???

Nzokanhyilu

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2007
Posts
1,078
Reaction score
101
Mimi naona watachemsha wakimchukua. Whats your take?
 
Tatizo la timu ya England sio kocha, ila hawana wachezaji wenye uwezo mkubwa, ndio maana hata wakienda nje ya ligi yao huwa hawaonekani. Kwa hiyo hata wamlete kocha gani ni bure tu. Let them start from the drawing board.
 
Tatizo la timu ya England sio kocha, ila hawana wachezaji wenye uwezo mkubwa, ndio maana hata wakienda nje ya ligi yao huwa hawaonekani. Kwa hiyo hata wamlete kocha gani ni bure tu. Let them start from the drawing board.

Na mind you hapo Mourinho hatakuwa na pesa wala uwezo wa kununua wachezaji kama alivyokua akifanya chelsia.Sidhani kama ataikubali hii post, he seems to be more interested in clubs management ambako anajua hata mambo yakienda vibaya katikati ya msimu, atatumia january transfer window kuweka mambo sawa.
 
Kweli, unajua mimi bado sijaamini kama Mourinho mkali kama waingereza wanavyompapatikia. Ila naona wanataka wa-risk waone kama kweli he is the special one.
lakini waingereza wanahitaji over-haul ya Academies zao. Najaribu kufananisha na Uholanzi, ambako hata kina Cruijff huwa wanapiga makelele kuhusu foreign players kujaa. Lakini Holland nchi ndogo na wanazidi kutoa wachezaji kila siku. Yaani system yao ya mpira ni bomba sana. CLub hata ndogo tu ya madaraja ya chini, inaweza ikawa na timu hata 30 hadi 60 kuanzia juniors mpaka veterans. Hapa UK, klabu nyingi sana sana unakuta wana timu 4 hadi 6 tu hivi. Jamaa wanapigia makelele foreign players, ukweli ni kwamba Youth system yao chovu chovu.
 
Mourinho ndio muarubaini wa timu ya uingereza, wakiweza wamchukue..yule kichwa bwana, sema hataki kuingiliwa. Hata akipewa timu ya bongo mambo yatanyooka. Timu inahitaji mwalimu mbunifu sio tu wachezji mahiri. Mwalimu mwenye uwezo wa kusoma mwelekeo wa mchezo na kufanya mabadiliko stratergically. Namheshimu huyo kocha sana.
 


Jose: I'll make England wait


He won't manage the England team well as his type of coaching is based on highly talented players of which England lacks.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…