Mourinho: Ningekuwa likizoni Brazil ningejua hakuna njia ya kuwazuia Manchester City

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Lukaku.jpg

Meneja wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amesema "angelikuwa likizoni Brazil au Los Angeles" iwapo angekuwa anaamini kwamba mbio za Ligi ya Premia msimu huu zimepata mshindi.

Alisema hayo baada ya klabu yake kulaza Bournemouth 1-0 Jumatano.

United walijikwamua kutoka wka kichapo cha Manchester City wikendi lakini hawakuweza kupunguza mwanya kati yao na City ambao wamo alama 11 mbele yao kwani vijana hao wa Etihad walilaza Swansea 4-0.

Romelu Lukaku ndiye aliyewafungia Man United bao hilo la ushindi kipindi cha kwanza.Mourinho alisema: "Mechi hiyo dhidi ya City ilikuwa kubwa, na ukishindwa hilo halisaidii juhudi zako za kujiweka sawa tena - ushindi husaidia, kushindwa hakusaidii.

"Bournemouth walikuwa wapinzani wakali na hali ilikuwa ngumu. Kama tungelifunga bao la pili tungetulia.

"Nimefurahishwa na alama hizo tatu. Walipumzika siku moja zaidi yetu, walikuwa sawa kutushinda baada ya kupumzika, hata kiakili kwa sababu mechi kubwa huwadhoofisha wachezaji zaidi.

"[Mbio za ligi] zitamalizika tu Mei. Kama zingekuwa zimemalizika sasa ningeenda likizo Brazil au Los Angeles."

Msimamo wa Mourinho ni tofauti na meneja wa Chelsea Antonio Conte ambaye amekiri kwamba itakuwa vigumu kuwazuia Manchester City.

United walikuwa wamecheza mechi 40 nyumbani bila kushindwa hadi walipolazwa na vijana hao wa Pep Guardiola Jumapili.

Chanzo: BBC Swahili
 
Ha ha ha ha ha
makocha huwa na maneno.....
last week alisema baada ya gemu ya asernal to game ya cska kipa sergio romelo ndio kipa bora #1 .....
 
Philosophy ya mourinho inatokana na vitu vitatu,..
1. Msimu huu wa Christmas match mbili kwa wiki,
2. Mkorogo wa FA CUP UEFA Champions League,
3. April-May relegation fight..

Hivyo vitu vitatu vina tabia ya kuchosha na kujeruhi wachezaji sana tuu.. Hapo ndipo panapompa mou kichwa kwamba ana kikosi kipana kuliko timu nyingi za EPL na ndio jeuri ya hiyo kauli yake kwamba mbio zinaishia MAY..

ingawa nilimsikia mchambuzi mmoja akisema ushindi wa city kwa utd ulisababishwa na kurudi kwa silver na kukosekana kwa pogba, siamini kwamba city inaweza kumaliza msimu bila kufungwa hata mechi moja na kutoa droo mechi mbili hivi kabla ya February..

Mimi ni mshabiki mnazi wa Man Utd, samahani kwa kuvutia upande wangu, ingawa nimejaribu niwezavyo kuichambua kauli ya mou nikiwa katikati bila kupendelea
 
Una haki ya kudhani hivyo. Lakini haki hiyo ya kudhani wanayo wapenzi wa Man City. Wao wanadhani kwamba Man U nao pia watafungwa japo mechi moja nyengine na kusuluhu japo mbili. Kwa hivyo hata kama City atafungwa na kusuluhu zaidi ya ulivyomtabiria, pengo la pointi za City zaidi ya Man U litabaki tu. Kwa maneno mengine, pengo la alama 11 ni sawa na mechi tatu na sare mbili, yaani Man U wanaweza kuliziba iwapo tu City wataboronga idadi hiyo ya michezo huku wao wakishinda mfululizo. Je, licha ya wembamba wa kikosi chake, City ina dalili za ubovu huo? Na je, licha ya upana wa kikosi chake, Man U wana dalili za ubora huo?
 
Philosophy ya mourinho inatokana na vitu vitatu,..
1. Msimu huu wa Christmas match mbili kwa wiki,
2. Mkorogo wa FA CUP UEFA Champions League,
3. April-May relegation fight..

Hivyo vitu vitatu vina tabia ya kuchosha na kujeruhi wachezaji sana tuu.. Hapo ndipo panapompa mou kichwa kwamba ana kikosi kipana kuliko timu nyingi za EPL na ndio jeuri ya hiyo kauli yake kwamba mbio zinaishia MAY..

ingawa nilimsikia mchambuzi mmoja akisema ushindi wa city kwa utd ulisababishwa na kurudi kwa silver na kukosekana kwa pogba, siamini kwamba city inaweza kumaliza msimu bila kufungwa hata mechi moja na kutoa droo mechi mbili hivi kabla ya February..

Mimi ni mshabiki mnazi wa Man Utd, samahani kwa kuvutia upande wangu, ingawa nimejaribu niwezavyo kuichambua kauli ya mou nikiwa katikati bila kupendelea
Nyie hamchezi iyo michuano?
 
Back
Top Bottom