Movie of the week: Wrath of Man

Movie of the week: Wrath of Man

Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2020
Posts
1,667
Reaction score
2,595
Fortico security walimtambua kama Patrick Hill kwenye kazi zilizohitaji usafirishaji wa fedha, aliajiriwa yeye kama mmoja wa wasindikizaji hao.

Kanuni ndogo tu, unafanyiwa mazoezi ya matumizi ya risasi, kujua kuendesha gari, na kukimbia ikibidi. Kwanini!, ni kwa sababu kila gari lilillobeba pesa nyingi kupeleka mahali palipohitajiwa, hazikufanikiwa kufika, zilitoka kwenye kampuni, zikaishia kwa wahuni..

Fortico security, kampuni ya kuaminika, ilishapoteza watu wake kwa kubisha kutoa hela kwa majambazi njiani, ikapoteza na hela zenyewe, sasa walielekea kuiteketeza na kampuni kabisa. Na hilo ndo lililowauma.

Leo pesa zilikabidhiwa kwake Patrick Hill, siku ya kwanza kazini, na siku ya kwanza kutekwa, dereva wake alipowaona majambazi, akajua kuwa Patrick ana bahati mbaya, au hana bahati kabisa.

Mshangao!, ndio, walishangaa wote waliokuwa ndani ya gari, Patrick Hill hapigi ili ukatibiwe, anakupunguza kwenye sensa ya watu na makazi, majambazi walihitaji muda kuziandaa risasi zao, walichelewa sana.

Wa mwisho alipigwa risasi ya kichwa akiwa anaomba msamaha asipigwe risasi kabisa, Patrick Hill ni mnyama, gari la kubebea pesa lilikuwa limepata mwenyewe, aliua huku anatabasamu, aliwaonesha wenzie kuwa yeye na kifo ni marafiki wa muda mrefu sana, hawatengani kizembe.

Alipokelewa kwa makofi kazini, akakaribishwa kwa bashasha ofisini, bosi hakuamini, alishazoea kuona gari pekee la hela lililorudi safari, ni lile lililotobolewa matairi kwa risasi, ila sio kuzikuta pesa wala watu wakiwa salama..ajabu hii!.

Akapewa safari nyingine, akabadilishiwa kiasi cha pesa, kama walifikiri kuwa ile mara ya kwanza ni bahati mbaya, walipaswa kufikiri tena. Safari hii walitekwa, na majambazi walivaa mask usoni, Patrick Hill, alishuka kwenye gari kama anaenda kuzungumza na marafiki zake wa muda mrefu, walipoiona sura yake midomo ilipoteza ulimi, kelele zilizima kama umeme uliokatika harusini, ni nani huyu!..
ambaye Akicheka ndo anakuua, haijulikani lini ana furaha, lini amehuzunika, na kwanini majambazi wanamuogopa!

Hargreaves, the boss of a crime syndicate, jason statham, yule fundi wa matial arts tuliemjua miaka ya nyuma, binadamu pekee mwenye tabasamu la maudhi.

Hajaja kwenye kampuni hii kuomba kazi ili afundishwe kuendesha gari, yeye anamiliki kampuni yenye magaidi na watu wenye roho mbaya kuwahi kuumbwa duniani, magari anayo.

Hajafika hapa kwa ajili ya kupelekwa kwenye mafunzo ya kupiga risasi, yeye bunduki kwake anazitengeneza mwenyewe, kaja kufanya nini sasa!

Ni Dougie, mtoto wake pekee wa kiume, alimpenda akampa moyo wake, moja kati ya siku za matembezi yao, Dougie alifia mbele ya macho yake.

Ni majambazi waliokuwa wamevamia gari ya Fortico security kwa ajili ya kuchukua pesa, waliwaua dereva na askari wake, mtoto wa Jason statham aliona tukio lile, wakampiga risasi kama shahidi.

Jason alipohitaji kwenda kumsaidia mtoto wake, na yeye aliadhibiwa, baba akapona, mtoto akafariki. Hiki ndo kilimfanya akaihitaji kazi kwenye kampuni ya usafirishaji pesa, ile ile iliyosababisha mwanae afe.

Na lengo lake lilitimia, siku ya kukabidhi pesa nyingi, ile timu iliyomuua mwanae ikapanga mbinu za kuiteka tena gari ya kampuni ile, walichokuwa hawajui ni kuwa.

Baba wa mtoto waliemuua miezi mitano iliyopita, ndo askari kwenye usimamizi wa gari hizi, majambazi wanahitaji pesa, Jason anahitaji kulipa kisasi cha kinyama. Ilipigwa vita ya kiume, inayowataka wanaume tu.

Ni mauwaji, taharuki, visasi, na usaliti, Jason statham tena, kwenye ubora wake wa mwaka 2021..

Wrath of man
Action thriller movie
I'm back
NINJA

©Kaisal Ally

193785497_1681587165357913_4536319325463219400_n.jpg
 
Dude kali hili, jamaa hana huruma anaua kama anatafuna karanga vile.

Ni nzuri hajawahi kuniangusha huyu mwamba.
 
View attachment 1811660
Sema jamaa aliyemuulia mwanae nae mwamba sana.🙌😂😂 Alivyomliza yule afande mwishoni.
 
Back
Top Bottom