The night of
Review 8.5/10
Hili ni bonge la season ambalo limenibamba sana..ni la kitambo kidogo 2016) uwezi jutia mda wako.Hili chuma ni lina "drama" na "crime"
Humu ndani kuna kijana asili ya kihindi, kwa majina yake "Nasir Khan".
Nasir khan anaalikwa kwenye party na rafiki yake wa shule.Mzee wake ni dereva Taxi,So usiku wa mwaliko anamvizia mzee na bi mkubwa wake wako chumbani anaiba funguo ya Taxi ya mzee na kutokomea nayo kuelekea kwenye party.
Njiani anambeba binti kama abiri,Safari yake ya kwenda kwenye party inaishia hapo anajipata yuko nyumbani kwa binti,akiwa kwa binti analewa na kuvuta madawa..
Wanaangukia kwenye kitanda wanafanya anasa,usiku mkali Nasir khan anashtuka ni mda wa kurudi nyumban na ameshachelewa,anarudi chumban anakuta binti kauwawa kifo cha kikatili sana...
Anachanganyikiwa,anaamua kutoroka kwa zile haraka haraka zake na wasiwasi anatoka apande Taxi ya babake bahati mbaya kasau funguo ndani,inabidi arudi na mlango umejiloki teyari kwa ndani..
Je atafanikiwa kuingia na kupata funguo yake?
Atafanikiwa kutoroka bila kukamatwa?
Hapo ndio mwanzo wa visa na mikasa...
Litafute ulicheki hutajutia mda wako