Now watching ASSASSINATION GAMES.
Mimi tangu niache kusema dushua dushua kipindi kile. Nkajua yamepita. Haya huku majukumuni nakutana na hii filamu ya bwana mkubwa Jean-claude van damme. Hapa anaigiza kama muuaji wa kukodishwa. (Contract killer) anapata kazi ya kumuua bosi mkubwa hapo ujerumani na upande wa pili kuna muuaji anaeitwa "flint" jina la kuigizia. Ambaye miaka michache iliyopita bosi huyo alimvamia na kumpiga mkewe hadi akapooza mwili wote.
Wote hawa wenye miraba sita kama sio mitano na van damme mwenye kifua kama meza wanaungana baada ya kujua wanataka kumuua mtu mmoja.
Wakati huohuo bosi wake van damme anafatwa na anaetaka kuuliwa (polo) na kumpa dili la kumtafuta anaetaka kumuua (flint) naye bosi anamfata van damme kumbadilishia kazi. Badala ya polo sasa amuue partner wake flint. Enjoy! A must see [ action, romantic, drama, thriller]