Movie ya Rahasya

Movie ya Rahasya

Johnny Sins

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2019
Posts
2,537
Reaction score
3,873
Image may contain: 6 people



Umri ulimwambia kakua..usichana ukapiga nae story kumshawishi awe na mvulana..akawa nae..akautimiza ukamilifu wake kiakili..baba dokta mama dokta..ayesha sachin aliishi kikamilifu kwenye maisha kamilifu..

..Anaamka saa nne anakuta kila kitu mezani..shida haikuthubutu kumfata..alichukua alichopenda bila kuomba..na aliomba akapewa alichoshindwa kukichukua..

..hana anachokosa..

..Leo alilala kama anavolala siku zote..ila hakuamka kama anavoamka siku zote..

...Kwenye mwili wake wa kike kulibaki uzuri tu bila roho..maiti yake imegundulika asubuhi,na asubuhi hii ndo nyumba ikajua kuwa imefiwa..nani kamuua ayesha?..

..Shingo yake imekatwa kiufundi kwa mtindo wa matibabu..na kisu kinachotumika kufanyia operesheni hospitali!..

..nani anaejua kutumia visu hivi kama sio babake na mama ake?ambao ni madaktari..baba kamuua mwanae?..kwanini?

...Nyumba ina askari nje,ndani kuna baba,mtoto,mfanyakazi wa kike na wa kiume..mama kasafiri..nani kamuua ayesha?

..Kwenye mkono wa marehemu kuna nywele ya babaake..kwenye kisu kuna alama za vidole vya babaake..baba analia hawezi kufanya hivo..mama karudi safari analia mumewe kamuulia mwanae..

..Upelezi unakamilika dr sachin anaingia hatiani..serikali inafunika kombe mwanaharamu anafanikiwa kupita...inasubiriwa hukmu..

...Ni shirika la haki za binadamu ndo lililompa ajira ya kurudia upelelezi paraskar..muhuni mwenye uwezo mkubwa wa matumizi ya fikra..C.B.I officer mwenye kesi za utata nyingi zilizofanikiwa..

..Paraskar anapenda kesi ngumu na kesi ngumu zinampenda yeye..analivagaa na hili..ila safari hii alikosea..

..Kila hatua aliyokuwa anapiga kuuelekea ukweli..alikuwa anausogelea mdomo wa kifo chake mwenyewe..password zote alizofungua zilikuwa na password nyingine ndani..ni kizaazaaa..

..Watu wote aliotegemea kuwahoji kuhusu hili aliwakuta wakiwa maiti kabla ye hajafika!..wauaji walikuwa hatua moja mbele yake..kila alichowaza wao walikiwaza kabla..

...Nyuma ya kifo cha Ayesha kuna mipango ya kisayansi iliyoundwa kwa ufundi wa hali juu na watu wanaoijua vizuri kazi yao..hakuna kilichofanyika kwa bahati mbaya..na hakuna kilichomuhusu babaake...ni nini kilifanyika?

..Ayesha kafa saa tano usiku na askari alikuwepo nje..na alieua hakutoka ndani..imekuwaje?..

...Wakati maswali yakipishana kwenye kichwa cha paraskar mpelelezi..anakuja kugundua kuwa dr sachin nae yupo matatani..na muda anaotaka kujua nini kinaendelea..

..ndipo wanapogundua maiti ya dr sachin ikiwa imekatwa kwa mtindo ule ule wa mwanae..what is this!..

..Nani atatue huu utata..kesi baada ya kesi..

..#Nani kamuua ayesha mahajan?!.

...Utashangaa ukiiangalia movie ukamjua muuaji..kama nilivoshangaa mimi!..

..#ONE OF DA BEST THRILLER MOVIE
#RAHASYA






CREDIT:Kaisal Ally
 
Hii si ni ile movie ambayo maiti inatubwa sitting room na kapeti inawekwa juu?
 
Back
Top Bottom