Johnny Sins
JF-Expert Member
- Nov 4, 2019
- 2,537
- 3,873
Wanasheria wa familia walipitisha tamko..maamuzi ikawa ni kugawa urithi..
..Kwamba mzee Richard croft amepotea na ameshindwa kupatikana..mtoto wake wa kike akawa ni kati ya wataopata sehemu ya mali za baba ake..
..Lakini akakataa..
..Lara Croft hakuamini kuwa baba ake kafa..alichojua amepotea..na aliepotea yoyote anapaswa kutafutwa..
...RIchard croft..mwanasayansi wa zama hizi..mgunduzi alieamua kuyaweka rehani maisha yake..ili akajue kilichohifadhiwa kwenye jiwe la kale..ndani ya Himiko..
..Safari yake aliyoondoka bila kuaga..ilimpeleka mythical Queen of Yamatai..kwenye kilele cha historia ya kale ndani ya japan..
...Miamba iliyosemekana kuna vitu vya ajabu vyenye manufaa kwa binadam...
..mzee richard croft alihitaji kuufanya ufundi wake wa sayansi awe ndo mgunduzi wa kilichokuwa kwenye hazina zile..
..Ni tomb stones...ambako inasemekana kufika hapo ni kuyaweka kwenye betting maisha ya kila kiumbe hai..
..Kuchagua kufa ikawa ni moja ya maamuzi aliyochagua mwanasayansi msomi richard..
..Lakini atimize kilichokuwa akili mwake..
...Akaiweka shule mbele..akaacha uoga nyuma..
...Richard croft..akajiona mussa..ila fimbo yake ikamkatalia kugeuka nyoka..
..Vitu alivyoacha nyumbani mzee Richard..ni pamoja na onyo kuwa binti yake achome moto kila aina ya uchunguzi aliokuwa akiufanya kabla hajaondoka kuhusu huko anapokwenda..
...Lara croft hakuchoma moto..akatumia uchunguzi ule ule wa babake kumtafuta alipo..
..Hong kong ikampokea kijasiri...Devil's Sea..dragon triangle..upande wa kusini mwa tokyo...ndipo yanapopatikana maji ya kasi yanayopeleka vyombo vigumu upande wa pili..
...Mwaka 1955 meli iliyoitwa Shinyo Maru No. 10 ilipotea..na tarehe 15 ikapatikana ikiwa salama..kasoro watu..
...Ni mkondo wa maji wa hatari..wenye maajabu ya hatari pia..
...Lala croft akaapa kumrudisha babaake nyumbani..iwe kwa heri au kwa shari..
..Na yeyote ataekaa kwenye njia yake kumzuia hilo...alikuwa anatia saini ya msiba wake mwenyewe..
..Mathias Vogel...kiongozi wa wanamaji makatili..ambae nae alikuwa kajua kuhusu faida inayopatikana kwenye yale mawe..
..Na alikuwa anajua kuwa mzee richard yupo huko..na yeye alitaka kufika ili akamshurutishe mwanasayansi yule amwoneshe kilichomo kwenye mawe..
...Lara croft anamtaka baabaake..Mathias Vogel..anataka kuionesha dunia utajiri wa kihistoria kupitia kichwa cha mzee richard kilazima..
...Akamkamata Lara..amtumie kama chambo kufika kwa babaake..
....Alikosea..
...Lara croft sio kama wanawake wengine..ni ninja kweli kwenye mwili wa kike...alichoapa kuhusu baabaake alihitaji kukitimiza..
..Ameacha mali mjini akaja porini..kurudi mjini bila ya kupata kilichompeleka aliamini ni kuikosea nia yake..
..Akafunga mkanda mwanamke akaingia vitani..
..Arudi na babaake au warudishwe maiti wote...
..Lara aliitoroka kambi ya mathias mbele ya macho yao..ukubwa wa msitu na maporomoko ya maji...
..Ndo viliwashangaza wanajeshi wa mathias..wakaamini kwa uanamke wa Lara..hawezi kufika chini akiwa hai..
..Lara croft..mtoto wa mzee richard..mwanasayansi mbobezi..
..Alifika chini akiwa mzima...na akaiambia akili yake jambo moja tu..
...Ni vita...ndio.. bike courier Lara croft..aliingia vitani..
..Richard hakuamini alipomuona binti yake..kombat mwilini..kachafuka usoni..mishale mgongoni...alilia.....
...Binti akamwambia baba nimekufuata wewe..na kuna washenzi wanakuja wanataka kukuua baada ya kuwafanyia usayansi wako..
..Mzee richard akafuta machozi..akamwambia binti yake mi nafanya sayansi we..wanyooshe..turudi nyumbani..
...Mathias Vogel...akaja na timu yake bila ustaarabu..akamkuta Lara croft..sio mtoto wa mwanasayansi tena..
...Ni mafia wa kike mwenye nia na babaake...
....Ilikuwa kazi..