Movie za Christopher Nolan hasa Inception na Tenet zinazingua sana

Movie za Christopher Nolan hasa Inception na Tenet zinazingua sana

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Nilikuwa naangalia movie ya Tenet. Sijaenjoi kabisa. Unaangalia movie lakini unakuwa kama unasolve puzzle bwana. Inception nayo ilikuwa hivyohivyo lakini afadhali hii ilikuwa na action nzuri.

Nyie wenzangu mmeenjoy Tenet?
 
rick-and-morty___confusing_and_stupid_like_inception.jpg
 
Uyo jamaa anatengeneza movie kama anacheza chess hajui kama sisi wengine ni vilaza.. Movie zake pekee ambazo nimezielewa mwanzo mwisho ni Batman Trilogy
 
Hizo filamu ni za kuangalia kichwa kikiwa kimetulia yaani ume relax na sharubati pembeni.
 
Hizo filamu ni za kuangalia kichwa kikiwa kimetulia yaani ume relax na sharubati pembeni.
Unaweza kusoma hesabu huku umerelax? Ndiyo hizi movie hasa hii tenet. Hii hadi nimegoogle na kwenda wikipedia ndiyo nimepata mwanga. Jina lenyewe, TENET ni fumbo. Hili linaweza someka toka kulia kwenda kushoto na toka kushoto kwenda kulia, kuonyesha jinsi movie ina deal na mambo ya time travel.

Sator_Square_at_Oppède.jpg
 
Ngoja niruke nayo nipime Uelewa wangu

Sito cheat kwa kutumia Google wala nini

Na nita-iangalia mara moja tu

Alafu nitaleta mrejesho
 
Ila mimi napenda matukio alivyoyapangilia kwenye Dark knight na Dark Knight rises
 
Hiyo ni kutokana na baadhi ya filamu zake kuwa na maudhui ya 'Thriller'. Filamu nyingi zenye maudhui haya zinaweza kukufanya ujihisi hivyo unavyojihisi. Unaweza kutazama filamu mpaka mwisho ukabaki unashangaa tu usijue ni kitu gani kimetokea ama tendo fulani limefanyika kwa sababu gani.

Hiyo TENET imechezwa na mtoto wa Denzel Washington. Huyu jamaa ni mmoja wa watu makini sana katika tasnia ya filamu ulimwenguni. Watoto nao wameamua kuiga fani ya mzee wao.
 
kuna interstellar pia kama hujatulia hutoielewa.

Inception nilianza kusoma plot kwanza baadae ndio nikiangalia movie.
Yenyewe pia ni ngumu kuelewa kama hutokuwa makini.
Kule mwishoni unaweza kudhani mr. cobb bado yupo ndani ya dream.
Tenet bado sijaiona.

Christopher Nolan ukichanganya na hans zimmer kwenye soundtracks basi hiyo movie lazima iwe decent.
Kama batman dark night trilogy.

Bongomovie wangekuwa wanafanya vitu kama hivi ingekuwa poa sana.
Sijui lini watafika viwango vya aina hii ukiondoa budget bado itahitaji akili na ubunifu wa kutosha.
 
Back
Top Bottom