Movies mbili zenye visa vitamu

Movies mbili zenye visa vitamu

SteveMollel

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
8,797
Reaction score
25,177
BEFORE I GO TO SLEEP.
c007b7c53bf3123920a553acaf45cfa9.png

Christine anapoamka asubuhi, anashangaa yupo mahali asipopafahamu na pembeni yake amelala mwanaume asiyemjua.

Anajaribu kuvuta picha lakini hamna kinachokuja kichwani.
ab94ef167f512348a2d112ec0b7d1c1f.png
Anaenda bafuni, humo anakutana na picha kadhaa ukutani, picha akiwa pamoja na bwana yule alomwacha kitandani.

Hivyo anaporudi, anamuuliza bwana huyu, wewe nani? Na vipi niko hapa? Bwana anasema yeye ni Ben, mumewe wa ndoa, na hapa ni nyumbani kwao.

Ben anamweleza alipata ajali ya gari miaka kumi ilopita hivyo akapoteza kumbukumbu zote, na tangu hapo kila anapoamka anakuwa mpya, mpya kichwani, hamna anachokumbuka hata kile alichoona na kukifanya jana yake.

Vuta picha, kila ukiamka unatoa maelezo kwa mkeo, wewe ni nani. Kwa siku saba za wiki, siku thelathini za mwezi, mia tatu za mwaka, sasa ni miaka kumi! Ungeiweza ndoa wewe?

Kwanza unaomba vipi cha asubuhi?
224c39145eb4b703953fc1d7331ff0a2.png
Ben anajiandaa na kwenda zake kazini, huku nyuma simu inaita na Christine anapopokea anakutana na sauti ya mwanaume anayejitambulisha kwa jina la Dr. Nash.

Dokta huyu amekuwa akimtibia kwa muda wote na anamwambia Christine kuna kamera ndani ya kabati lake, kamera hiyo ina rekodi ya mambo yalopita basi itamsaidia kuzivuta kumbukumbu.

Kutazama, kweli kuna kamera. Kuangalia, ina vitu kadhaa lakini si vya muda, ni vya majana na majuzi, hivyo kujifahamu zaidi anaona ni vema akutane na dokta yeye mwenyewe.

Kwa dokta anapata habari mpya, habari za kushangaza. Dokta anamweleza chanzo cha yeye kupoteza kumbukumbu ni shambulio la kichwa.

Bwana mmoja alimshambulia tena si mara moja wala mbili, alimpiga tena na tena kisha akamtelekeza akiwa na hali mbaya sana.
65470ba5af8bc396508243d11d63aab2.png
Kwa lengo la kuvuta kumbukumbu, Christine anaongozana na dokta mpaka sehemu alipotelekezwa baada ya shambulizi hilo.

Mahali hapo wanakutana na shahidi na inabainika Christine alikutwa amejawa na damu kichwa kizima, pia mbali na shuka la hoteli alilokuwa nalo, alikuwa yuko uchi wa mnyama!

Isitoshe Dokta anasema, kwa mujibu wa vipimo, Christine alikuwa ametoka kufanya mapenzi muda si mrefu kabla hajashambuliwa.

Sasa Christine anazidi kuchanganyikiwa.

Nini kinaendelea? Alifanya mapenzi na nani? Nini kilitokea? Mbona mumewe alimwambia kuwa alipata ajali ya gari?

Yani mambo ni mengi.

Anarudi nyumbani na kwa kutumia ile kamera ya kabatini, anarekodi yale yote aliyoyajua leo hii ili kesho akiamka basi asianze tena upya.

Anapomaliza anaificha kamera hii kama alivyoelekezwa na dokta, aiweke kamera mbali na mumewe, Ben.
Screenshot_20240522-231551.png
Sasa kadiri muda unavyoenda, Christine anazidi kubaini vitu zaidi na anavirekodi vitu hivyo kwenye kamera yake.

Lakini kadiri anavyorekodi na kuvipitia visa hivi basi anazidi kuzama ndani ya shimo.

Kuna vitu vingi mumewe anavificha.

Na pia kuna vitu vingi haviko vile anavyoambiwa na watu.

Lakini vitu hivi akivijua vitamwacha salama?
Screenshot_20240522-231515.png

MEANDER

f235883c88b6a9195c8c18c2745ccd37(1).png
Kuna mwanamke mmoja amejilaza katikati ya barabara, hatujui anaumwa ama lah, ila gari linapokaribia, anasimama mwenyewe na kusogea kando ya barabara.

Mara gari hili linasimama pembeni yake kisha dereva anampatia lifti mwanamke huyu. Wanatambulishana kwa majina ya Lisa na Adam.

Mbali na jina, unaweza ukamtambua Adam kwa tattoo ya msalaba mkono wake wa kuume.

Basi safari inaendelea, na hii kampani ya Lisa inamfanya dereva (Adam) apate mtu wa kuongea naye, hivyo wanazungumza hiki na kile.

Katika maongezi haya, Lisa anamtaja mtoto wake aliyefariki, jina lake Nina. Anasema kama angalikuwa hai basi leo hii angalikuwa na miaka tisa.

Muda kidogo, Lisa anawasha redio ya gari na mara anasikia ripoti ya mwanaume mmoja aliyeua watu wawili.

Ripoti hiyo inamfafanua muuaji kwa sifa zake, ila ajabu sifa hizi zinawiana kabisa na bwana huyu aliye pembeni yake katika usukani.

Ikiwemo hii tattoo ya msalaba mkononi!

Lakini kabla hajafanya kitu, Adam anakamata breki ghafla, Lisa anajigonga kwanguvu kwenye dhasboard na kupoteza fahamu.

Anapokuja kuamka yu kwenye chumba kidogo kisichojulikana kipo wapi. Mkononi anakifaa kidogo kinachotoa mwanga wa njano.
67f1b048830e4d34ff1429942d8c5b48.png
Baada ya muda kidogo, mlango unasogea anaona tundu la njia nyembamba mithili ya pipa lililokatwa mdomo (a tunnel), anaingia humo kwa kutambaa na mara mlango unajifunga asiweze kurudi tena chumbani.

Hapo ndo' kifaa cha mkononi mwake kinawaka. Alarm inalia. Na muda wa dakika 11 unaanza kusoma kushuka chini.

Anatakiwa kufanya nini?

Ndani ya njia hii nyembamba, kuna jaribu moja kwenye kila section. Jaribu la mauaji. Jaribu ambalo una dakika kumi na moja tu kulimudu la sivyo unakufa.
044f5b7978c285073e075cf3ec34d4d8.png
Majaribu haya ni mitego ya kila aina na yanakuja na kila hofu.

Hivyo Lisa anajikuta ana kazi ya kupambania uhai wake ili akajue ni kwanini aliwekwa humu? Waliomweka wanataka nini?

Na mwisho, kuna mahusiano gani na kifo cha mtoto wake, Nina?

Tafuta popcorn, enjoy.
 
Attachments

  • 9d4406aedb4ae9a827b8d7d584c02974.png
    9d4406aedb4ae9a827b8d7d584c02974.png
    118.7 KB · Views: 24
Ongezea na zinginezo mkuu, Mimi NIPO hapa nimezielewa HIZO 2 za kuanzia
 
Before I go to sleep nimeielewa sana
 
Back
Top Bottom