Moyo kwenda mbio

Moyo kwenda mbio

kinjo

Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
69
Reaction score
33
Habari wakuu,

Naomba msaada wa mgonjwa alienda kupima ecg akaambiwa ana short pr interval naomba kujua matibabu yake na kama inatibika na kua katika hali ya kawaida.

Shukrani
 
Hiyo moyo kwenda mbio ndio kwenye ECG imeonekana short PR interval . Wajawazito/ watoto na baadhi ya watu huwa na short PR na wanaishi maisha yao kawaida .

Nadhani hospitali kabla ya kufanya hicho kipimo kuna maelezo walichukua ili kujua nini chanzo cha huo moyo kwenda mbio .

Kuna shida ambazo rahisi kutibika na nyingine zitahitaji utumie dawa kwa muda mrefu kama sio maisha yote .

Jitahidi ufuate maelekezo unayopewa na wataalamu .
 
Habari wakuu,

Naomba msaada wa mgonjwa alienda kupima ecg akaambiwa ana short pr interval naomba kujua matibabu yake na kama inatibika na kua katika hali ya kawaida.

Shukrani

Pole kwa kuuguza.
Mtoa mada zingatia ushauri hapo juu:
1: Tafsiri halisi ya shida ya mgonjwa inategemea muunganiko wa dalili alizonazo mgonjwa. Hii itategemea pia na kama chanzo ni moyo wenyewe au kitu toka nje alichochukua mgonjwa kama dawa za kutibu ugonjwa mwingine au tatizo la sehemu nyingine ya mwili kama upungufu wa damu.

2: Tafsiri halisi ya kuhitaji tiba au kutokuhitaji tiba inategemea na chanzo lakini pia kiasi cha tatizo. Kuna watu hili huchukuliwa kama suala la kawaida kama ilivyoelezwa hapo juu. Pia tiba inaweza kuhusisha kutibu chanzo cha tatizo nje ya moyo kama kwenye 1 hapo juu.

2: Fanya majadiliano na mtoa huduma wako ili kujua maoni yake juu ya shida halisi ya mgonjwa na matazamio ya mgonjwa kurejea vyema.

3: Msisitize mgonjwa kufuata taratibu za kimaisha kadri atakavyokuwa ameelekezwa kwani ni muhimu sana.
 
Back
Top Bottom