Hiyo moyo kwenda mbio ndio kwenye ECG imeonekana short PR interval . Wajawazito/ watoto na baadhi ya watu huwa na short PR na wanaishi maisha yao kawaida .
Nadhani hospitali kabla ya kufanya hicho kipimo kuna maelezo walichukua ili kujua nini chanzo cha huo moyo kwenda mbio .
Kuna shida ambazo rahisi kutibika na nyingine zitahitaji utumie dawa kwa muda mrefu kama sio maisha yote .
Jitahidi ufuate maelekezo unayopewa na wataalamu .