“Sababu ya MOYO watu muhimu wamepotea”
Nawasalimu wote wana ukurasa huu wa stories of change na wana Jamii Forum kwa ujumla. Leo kwa mara nyingine nawaletea habari nzuri ambayo haijasahulika sana kijamii ila natamani kwa pamoja tuelewe maana maarifa ni silaa muhimu sana na mimi wala hata sio mchoyo, KARIBU.
Nalazimika kusema hili si tunaelewa kabla ya yote maombi ni jambo la muhimu na la kiungwana basi ukipata bahati ya kupitia hili andiko usisahau kulizawadia kwa kulipigia kura yako muhimu na pia ukurasa wa maoni, maswali na mengineyo hupo wazi. KARIBU.
MWANZO
Kama wengi tunavyoamini MOYO ni kiungo muhimu cha mwili wa mwanadamu na viumbe wengine pia ambapo wengi tuna Imani kubwa kuwa bila MOYO hakuna maisha kwa Imani zetu hii ni kweli ila kwa bahati mbaya watu tulio wengi MOYO hatuupi malipo yanayopaswa kutokana na kazi zake za kipekee na muhimu sana kwa maisha yetu. Basi leo nimetumwa na MOYO kuwapa huu ujumbe muhimu kutokana na maumivu ya MOYO ya kila siku hapa swali la kujiuliza, Je unautendea moyo wako yaliyo mazuri au hapana basi tembea na mimi katika andiko hili makini.
Kuna msemo unasema jeraha ni jeraha tu basi leo nakusogezea sababu za majeraha ya moyo. Lishe duni limekuwa tatizo kubwa duniani hasa katika nchi ambazo zimepewa jina la nchi zinazoendelea ambapo wananchi wengi wa hizi nchi ushindwa kupata vyakula bora na vyenye lishe ambavyo kazi yake kubwa huwa ni kuufanya mwili kuwa imara hivyo hivyo kuufanya MOYO kuwa imara na kukwepa baadhi ya majeraha mfano upungufu wa kula vyakula vyenye utajiri wa madini, protini na wanga kwa kiasi hufanya mwili kukosa nguvu za kupambana na mashambulizi yanayohusiana na MOYO hivyo kufanya MOYO kupata majeraha.
Kula chakula kingi muda mchache kubla ya kulala najua tuliowengi tutashangaa kama kweli hili ni tatizo ambalo linaweza kusababisha majereha au matatizo ya MOYO basi ukweli ni hivi huu utaratibu una shida mahali maana kula chakula kingi kabla ya kulala upelekea mabadiliko ya kikemikali ya chakula kuwa kiasi kidogo na uchukua muda mrefu hivyo kupekea utendaji mdogo wa kazi mwilini na baadae kupelekea ongezeko lisilo la kawaida la uzito wa mwili. Ongezeko la uzito wa mwili upelekea kutengenezwa kwa mafuta mwilini ambayo ujibanza katika kuta za mishipa ya damu hivyo kupelekea kupungua kwa kipenyo cha mishipa na muda mwingine kuziba kabsa hivyo MOYO hutumia nguvu kubwa kufanya kazi yake ya kusukuma damu hivyo husababisha majereha na matatizo ya MOYO.
Kutofanya mazoezi mara kwa mara, hapa najua kuna watu tunajiuliza na kujipa MOYO kwa kusema kuwa maisha yetu ya kila siku ni mazoezi tosha sikatai ila kila siku zinavyozidi kwenda wagonjwa wa magonjwa ya MOYO wanazidi kuongezeka basi hii inaonyesha kuwa lazima tuangalie upande wa pili wa kufanya mazoezi rasmi hili tuweze kuwa na afya njema na kuupunguzia moyo majeraha hivyo kupunguza uwezekano wa kupunguza magonjwa ya moyo ambayo kwa kiasi kikubwa husababisha na ongezeko maradufu wa uzito wa mwili utokanao na kula sana vyakula vya wanga na mafuta.
Kutokana na mabadiliko ya kiasili ya binadamu kuna matatizo ya MOYO hutokana na kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi, baadhi ya watu hupata haya magojwa ya MOYO wakiwa wadogo sana kwasababu ya kurithi vinasaba ambavyo hubeba haya magojwa na kwa bahati mbaya magojwa ya MOYO ambayo husababiswa kwa njia hii ni ngumu kuyadhibiti maana hutokea kutokana na historia ya familia hivyo mtu akizaliwa kwenye familia yenye utamaduni wa magonjwa ya MOYO ni muhimu kwenda kumuona mtaalam wa Afya ya MOYO ili kuweza kuelewa jinsi ya kuishi na kupunguza matatizo ambayo yanaweza kutokea kwa sababu ya kiasi kidogo cha elimu juu ya magonjwa ya kurithi ya MOYO.
Katika jamii zetu magonjwa ya moyo yamegawanyika katika makundi mbalimbali kuna magonjwa ambayo huathiri zaidi mishipa ya damu mengine huathiri zaidi mapigo ya moyo na ugonjwa wa MOYO maarufu ukiwa ni moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure). Pia kuna ugonjwa wa moyo kutanuka, ugonjwa wa misuli ya MOYO kushindwa kufanya kazi vizuri, shiniko la damu, shambulio la MOYO pia kwa kumalizia na ugonjwa wa chembe ya moyo ambapo mgonjwa wa ugonjwa huu hupata maumivu katika upande mmoja wa moyo akiwa amekaa au anapanda au kushuka ngazi za nyumba.
TUFANYE NINI?
Kuna msemo pendwa wa kinga ni bora kuliko tiba hivyo nashauri sana kufata kanuni za afya na kula vyakula vya mafuta na wanga kutoka na maelekezo ya wataalamu wa afya muhimu tusisahau mazoezi ambayo yatafanya miili yetu kuwa imara na kutuepusha na magonjwa ya MOYO ambayo yapo kwenye kundi la magojwa yasiyoambukizwa ambayo ni hatari na hudumu kwa muda mrefu maana mtu huweza kuishi nayo kwa muda mrefu.
Ndugu unapoona dalili zifuatazo wahi kituo cha kutolea huduma za afya ukaonane na mtaalam wa magojwa ya MOYO. Kwenda mbio kwa mapigo ya moyo kuliko kawaida, kuchoka haraka kutokana na mwili kuwa dhaifu, maumivu kwenye sehemu za juu za mwili (kuanzia tumboni) kwa kingereza yakiitwa referred pain, kuvimba sehemu mbalimbali za mwili kama miguu, tumbo na miguu kutokana na kujaa maji. Dalili nyingine ikiwa ni kushindwa kupumua vizuri mtu unapolala chali.
Kutokana na magonjwa ya MOYO tumepoteza watu wengi ambapo magonjwa ya moyo husababisha vifo vingi kila mwaka na maelfu ya watu wakipata magonjwa mengine kama kiharusi hivyo kupelekea kupungua kwa nguvu ya taifa.
Nachukua nafasi hii ya pekee kutoa salamu zangu za pole kwa wote waliopoteza ndugu zao na wapendwa wao kwa sababu ya magonjwa haya ya MOYO Mungu alaze roho zao pema peponi.
AMINA!!!

Attachments
Upvote
1