SoC03 Moyo wa Chuma

SoC03 Moyo wa Chuma

Stories of Change - 2023 Competition

Fide Simbili

New Member
Joined
Jul 26, 2022
Posts
4
Reaction score
4
Screenshot_20230620-190453~2.jpg




Kama tunavyofahamu kazi kubwa ya moyo ni kusukuma damu, moyo huu umekua tofauti katika kufanya kazi zake.

Tazama moyo huu umegawanyika katika Makundi makuu mawili, kundi linaloonekana kunawiri na ni kundi ambalo linawavutia watu wengi wautizamao.

Pia lipo kundi ambalo limeweka kutu na linaonekana kuchakaa bila mvuto wowote machoni Kwa watu.

Tizama moyo huu wa CHUMA ni moyo ambao unawashangaza watu wengi kutokana na CHUMA kuonekana kua stahimilivu lakini Bado kinachakaa vibaya na kuoza.

Tizama kundi kubwa la CHUMA kinachoonekana kuukuu linazidi kuongezeka siku Hadi siku, linazidi kukata tamaa ya kuendelea kuishi kutokana na uchakavu wake, uchakavu wa mazingira yake yanayowazunguka, uchakavu na ugumu wa kupata mafuta mazuri yatakayowapa mwangaza na kuchanua.

Hivi ndivyo Makundi haya mawili yanaishi maisha ya kubaguana, maisha ya kutokusalimiana, maisha ya kutokujaliana , Makundi haya ya moyo huu wa CHUMA yanatengenezwa, vita vikubwa kati Yao vinazidi kutanda siku Hadi siku.

Tizama Huruma imepotea, na ndivyo Makundi haya yanasababisha wengine wengi kuogopa na kukimbia porini kujificha.

Ndivyo wanavyokosa uhuru wa kujisemea, uhuru wa kujieleza na uhuru wa kusimamia Mali zao kutokana na ukata unaozidi kuwazunguka siku Hadi siku.

Kila wanapowatizama wenzao wanaishia kusema ...
"Tizama moyo wao unapendeza" wanaishia vyema, wanakula vyema , wanaendesha na kumiliki magari mazuri,

Moyo uliojaliwa kutamani, moyo uliojawa watu wachache ambao matumbo Yao Yako Mbele na kushindwa kutambua hao wanyonge ndio waliofanya wawe apo, wafike apo na wapige Kile wanachotaka.

Tizama Kijiji Cha Giza watu wanaelimika siku Hadi siku, akili zinaniimarika, wanatafuta mtu muhimu ambaye atasimama na kuwasemea.

Magari yanazunguka Kijiji Cha Giza, vinywaji vinasambazwa kuwapumbaza wanyonge ambao akili zao Bado zinafungwa na kishawishiwa na maneno matamu yaliyopambwa na nyimbo nzuri ndani yake.

Na hivi ndivyo Giza linasogea na kua Giza Nene zaidi machoni kwao, ahadi zinatolewa, watu wanaaminiwa na kukabidhiwa gurudumu ingali likiwa Bado ni zima, mwisho wake linatudi, tairi zote zimechomoka, vifaa muhimu vyote vimepotea.

Uoga ondoeni.
Tazama uoga ni Umasikini, uoga unalaza fikra na maamuzi ambayo yangejenga na kukivusha Kijiji hiki hata katika mwanga.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom