Mpaka mechi inaisha hajagusa hata mpira, Dollo alimaanisha nini?

Mpaka mechi inaisha hajagusa hata mpira, Dollo alimaanisha nini?

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
NI SANAA AU UTELEZI?

Anajulikana kama DOLLO MOSSES TMK HALISI.
Nilimfahamu toka enzi za Radhia, Inahitaji roho ya chuma kuishi na watu vizuri na ngoma nyingine za Wachuja Nafaka na TMK WANAUME.

Sasa baada ya TMK kumeguka mapande mawili makuu, Nature akajitoa na kuunda TMK WANAUME HALISI huku Dollo AKIWEMO na andiko letu limejikita katika wimbo uitwao TATU BILA
Humo ndani, Dollo anasema;

"MPAKA MECHI INAISHA HAWAJAGUSA HATA MPIRAAAA"
Kiuhalisia, timu inayofungwa inatakiwa iuanze mpira, Sasa hii timu ilifungwa magoli matatu na haikugusa mpira? Mpira haukutoka kwamba warushe? Hakukuwa na faulo yoyote?
Ahh! Sijui nimewaza kwa sauti

Kisanaa, inaweza kuwa ni mbinu iitwayo Mbalagha (Hyperbole, overstatement, or exaggeration)

Je, Dollo aliikusudia hii au kalamu iliteleza?

1683265785610.jpeg
 
Wavuta mabangi wanajiimbiaga tu lolote wao wanaona linawezekana

Kiuhalisia alimaanisha hyo game hao waliofungwa walikuwa wamezidiwa sana yaan ni ile umiliki wa mpira unakuwa 80% kwa 20%
 
Back
Top Bottom