Mpaka sasa nimepoteza $300 kwenye forex

nusuhela

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
5,915
Reaction score
7,210
Tangu niijue hii biashara ya forex kupitia Uzi wa Ontario, ni takribani miezi 7. Sikuwahi kusoma wala kupitia mafunzo yoyote Yale. Wala sinaga mentor.

Nilipoona Uzi wa jamaa na nikajua kuna uwezekano wa kupiga hela, nilienda moja kwa moja google kusearch nilichokisoma kutoka jf. Nilikutana na maelezo mengi sana. Nili download plattform na nikaanza kufanya demo. Japo nilikua sijui una place vipi order, lakini kwa kupitia video za YouTube, niliweza kujua. Nilinda na demo kwa takribani wiki mbili, nikaona napoteza muda. Nikaamua kufungua real acc ambayo nilianza nayo kwa kupata hasara. Kadri nilivyokua napata hasara, ndivyo nilivyokua najifunza.

Naweza sema nimejifunza vingi kwa muda huo wa miezi 7 hadi sasa. Nimeshaunguza acc si chini ya 10. Ambazo kwa jumla ni kama $300. Siwezi ongopa, mpaka sasa bado sijaanza kula faida za forex japo naamini baada ya miezi 2 nitakua nimerudisha hela zote kwasababu nimefikia hatua nzuri.

Nilivyojifunza kuhusu forex ni
1. Sio lazima Ku trade kama silielewi soko la wakati huo

2. Nifungue trade nikiwa na uhakika wa ninachokifanya.

3. Nibalance lot size kutokana na kiasi cha mtaji wangu

4. Nisifungue trade zaidi ya 1

5. Nisisahau kuweka SL

6. Nisiwe na tamaa na niweze kucontrol emotion

7. Sio kila pair naweza Ku trade

8. Hiyo loss ya $300, ni gharama ya kujifunza forex

Ahsanteni sana
 

hekooooooo

cc: francis-da-don
 
Hapa usitudanganye. Unachofanya ni kuwashawishi watu wajiunge huko. Hivi kama kuna mipesa hiyo mingi nje nje kwa nini mnatumia nguvu nyingi kutushawishi ma Laggards?
Mkuu samahani kama huelewi maana ya ushawishi.

Ipo hivi, watu wajiunge au wasijiunge, haitaniongezea wala kunipunguzia chochote. Ninachofanya mimi ni kuleta mrejesho wa nilichojifunza kupitia jf
 
Hapa usitudanganye. Unachofanya ni kuwashawishi watu wajiunge huko. Hivi kama kuna mipesa hiyo mingi nje nje kwa nini mnatumia nguvu nyingi kutushawishi ma Laggards?
Si ndo hapo
 


Angalau umekuwa mkweli... Kama umeliwa Usd 300 inamaanisha uliweka zaidi ya hapo.

Kitaalam, wanasema unatakiwa kuliwa 2% ... Kama hiyo Usd 300 inawakilisha 2% uko vizuri.

Kama siyo, unabidi kujifunza zaidi.

Kingine unachohitaji ni psychology of forex trading .... hii unaihitaji sana, maana umeanza sasa kuonyesha emotion... unapoanza kutrade kwa emotion, utaloose zaidi ya hiyo Usd 300.

Naamini uko katika emotion, kwa sababu inaonekana una hamasa ya kutaka kupata hela, hapo ndipo risk ya forex trading inapokula a/c yote.

Be careful.
 
Mkuu umenichekesha sana. Umenikumbusha msemo mmoja unaohusu Forex trading unasema hivi; "Don't ever trade haphazardly".
 
hatukomi tu!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…