Ukimpata mpenzi aliye ubavu wako wa kweli utajua tu! Yaani hakusumbui, anajua nini unataka kwa wakati gani, anajua wapi kwa kulia na wapi pa kucheka, mkikosana mnasolve kwa ulainiii bila mikelele kama mbuzi.
Ukivamia ubavu wa Kondakta napo utajua tu kila siku kelele, mikwara, matusi, utajua tu kwamba umeweka tairi la trekta kwenye Corolla, mambo hayaendi.
Muombe sana Mungu maana kuuvizia ubavu wako hadi uupate ni sawa na kupata siti kwenye gari la Mbagala, fulu taiming!